Wakati joto la Urais mwakani likizidi
kuongezeka nchini, Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samwel Sitta
ameweka wazi kuwa hana nia ya kuwania Urais kwa kutumia kigezo cha
kuongoza Bunge hilo maalum.
Akizungumza wakati wa kufungua kikao cha
thelathini na moja cha Bunge Maalum la Katiba ambalo limeanza kupokea
taarifa za kamati zake, Sitta hata hivyo alisema atakuwa tayari kufanya
hivyo kama wananchi wataona anafaa kwani wao ndio wenye dhamana ya
kuchagua mtu wanayetaka awaongoza.
“Wengine wananikejeli, wanasema kwa shughuli hii
naonesha sifai Urais, me sijaomba Urais,” alisema Sitta na kufuatiwa na
idadi kubwa ya makofi bungeni hapo.
Sitta aliongeza: “Naifanya kazi hii kama
Mwenyekiti wa Bunge la Katiba basi, lakini nasema wanaochagua ni
wananchi, inawezekana mwakani, wananchi wa Tanzania wakatamani mtu
mzima, aliyetulia na muadilifu, kama itakuwa hivyo wajue tupo na sisi
wengine.” Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz