Umati wa watu waliohudhuria
maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
yanayoendelea hivi sasa katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam,
maonyesho haya yanajumuisha shughuli mbalimbali zikiwemo maonyesho.
Maadhimisho haya yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoaka mataifa
mbalimbali (Picha na Awadhi Ibrahim)
Viongozi wa nchi Saba tajiri kwa
viwanda duniani G7 wamekubaliana kuongeza vikwazo zaidi kwa Urusi
ambapo wamesema imezidi kuifanya Ukraine isitawalike.
Ikulu ya White House ya Marekani imesema
wataanza kuweka vikwazo hivyo haraka iwezekanavyo kuanzia siku ya
jumatatu na wanatarajia kulenga biashara za binafsi na ambazo zina
uhusiano na Rais Vladimir Putin wa Urusi.Wametoa wito kwa Urusi kuacha mipango yake kijeshi ya siri kwenye mpaka na Ukraine.
Kwa upande mwingine viongozi hao wa nchi saba tajiri duniani wameisifu Ukraine kwa jinsi walivyojizuia kwa kupanda na wapiganaji waasi.
Serikali ya Ukraine imesema inahofia kuwa Urusi ina mipango ya kuivamia. Hata hivyo Urusi imesema nchi za magharibi zina mipango ya kuteka kuitawala nchi yao.