Wednesday, August 27, 2014

WATOTO 984 WAOZESHWA KWA NGUVU, 1628 WAKEKETWA TARIME...!!!

Baadhi ya washiriki katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike zitakazoendeshwa mkoani Mara. Uzinduzi huo umefanywa na mjane wa hayati Nelson Mandela, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca Michel Trust, Bi. Graca Michel leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike zitakazoendeshwa mkoani Mara. Uzinduzi huo umefanywa na mjane wa hayati Nelson Mandela, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca Michel Trust, Bi. Graca Michel leo jijini Dar es Salaam

Mjane wa Hayati Nelson Mandela, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca Michel Trust (GMT), Bi. Graca Michel (kulia) akishangilia baada ya kutuma ujumbe mfupi kwa njia ya simu za viganjani kwa simu zote zilizosajiliwa nchini Tanzania ikiwa ni ishara ya uzinduzi kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike zitakazoendeshwa mkoani Mara.
Mjane wa Hayati Nelson Mandela, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca Michel Trust (GMT), Bi. Graca Michel (kulia) akishangilia baada ya kutuma ujumbe mfupi kwa njia ya simu za viganjani kwa simu zote zilizosajiliwa nchini Tanzania ikiwa ni ishara ya uzinduzi kampeni za kupinga ndoa za utotoni kwa watoto wa kike zitakazoendeshwa mkoani Mara

Mjane wa Hayati Nelson Mandela na Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca Michel Trust (GMT), Bi. Graca Michel akimbusu mmoja ya watoto wa kike kutoka Mkoa wa Mara kuonesha ishara ya upendo katika uzinduzi huo.
Mjane wa Hayati Nelson Mandela na Mwenyekiti wa Taasisi ya Graca Michel Trust (GMT), Bi. Graca Michel akimbusu mmoja ya watoto wa kike kutoka Mkoa wa Mara kuonesha ishara ya upendo katika uzinduzi huo. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

WANANCHI WAKATAA FIDIA ILI KUJIPATIA UMEME

Displaying Mbunge wa Jimbo la Ludewa, Deo Filikunjombe (mwenye shati la kijani) akifukia udongo kwenye shimo wakati wa kusimamisha nguzo ya umeme kwenye kijiji cha Nindi kwa ajili ya kusambaza umeme vijiji.JPG
Filikunjombe mwenye shati la kijani akishirikiana na wananchi kufukia nguzo 
Displaying Mafundi wa Shirika la Umeme Tanzania wakiwa wamebeba nguzo ya umeme wakipeleka kusambaza kwenye mashimo yaliyochimbwa katika kijiji cha Nindi, Kata ya Lupingu wilayani Ludewa. (Picha na Michael Katona).JPG
Vijana wa TANESCO wakiwa kazini
IMG_5343_f8d22.png
Kazi na dawa Filikunjombe akiwa na kihifadhia chakula (Hot port) lenye karanga baada ya njaa kumkabili
IMG_5294_f599f.png 
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

URAIS 2015 WAIBOMOA BONGO MUVI




KUMEKUCHA! Baada ya kuwepo kwa misuguano ya chini kwa chini kati ya viongozi na wanachama wa kundi la waigizaji wa filamu la Bongo Movie Unity, sasa siri imefichuka kuwa baadhi ya watu wanaotajwa kuwania kuteuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) ili wagombee urais mwakani, ndiyo wanaolibomoa kundi hilo kutokana na fedha wanazodaiwa kuzitoa.

Mwenyekiti wa Bongo Muvi, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’.
Baadhi ya waigizaji wenye ushawishi katika kundi hilo waliliambia gazeti hili juzi kwamba, dhambi kubwa inayolitafuna kundi hilo ni kambi za kisiasa zinazoratibiwa na makada wawili wanaoonekana kuwa na ushawishi ndani ya CCM ambao wanatajwa kutaka kumrithi Rais Jakaya Kikwete.


“Unajua hapa Bongo Muvi kuna watu wamejikita moja kwa moja katika hizi kambi ambazo kuna waheshimiwa hawa wawili (majina tunayo) ndiyo sababu kuu ya watu wengine kufikia kujiuzulu kwa hoja kuwa wanatumika kwa manufaa ya mtu,” alisema mmoja wao aliyeomba hifadhi ya jina lake. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

DI MARIA ASAINI MIAKA 5 MAN U

WINGA Angel di Maria amejiunga rasmi na klabu ya Manchester United kwa ada ya pauni milioni 59.7 kwa mkataba wa miaka mitano.

Angel di Maria akipozi na Meneja wa Manchester United, Louis van Gaal.
Di Maria amekamilisha usajili huo leo usiku na atakuwa akilipwa pauni 200,000 kwa wiki nyuma ya Wayne Rooney anayelipwa zaidi klabuni hapo.
Staa huyo aliyetokea Real Madrid amevunja rekodi ya Ligi Kuu ya England kwa uhamisho wake wa bei ghali. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Di Maria akiwa na jezi ya Man U.
Baada ya kukamilisha usajili huo, Di Maria alisema : 'Manchester United ndiyo klabu pekee ambayo ingeweza kunifanya niondoke Real Madrid'
Di Maria anaungana na wachezaji wengine wapya klabuni hapo kama Marcos Rojo, Ander Herrera na Luke Shaw.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMATANO AGOSTI 27, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.


.
.
.
.
.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

UKRAINE NA URUSI ZAFANYA MAZUNGUMZO

Marais Vladmir Putin wa Urusi(kushoto) na Petro Poroshenko wa Ukraine(kulia) wakikutana Mensk, Belarusse tayari kwa mazungumzo
Marais wa Urusi na Ukraine wamekuwa na mazungumzo ya kwanza ya moja kwa moja kuhusu mgogoro wa eneo la mashariki mwa Ukraine, lakini inaonekana hakuna welekeo wa mgogoro huo. Kiongozi wa Ukraine Petro Poroshenko amesema "mpango" utaandaliwa haraka iwezekanavyo kumaliza mapigano kati ya majeshi ya Ukraine na waasi wanaotaka kujitenga.
Rais Vladimir Putin wa Urusi amesema nchi yake itasaidia katika mazungumzo, lakini suala la usitishaji mapigano ni la Ukaraine yenyewe. Ukraine imekuwa ikiishutumu Urusi kwa kuwapatia silaha waasi, madai ambayo yanakanushwa na Urusi.
Kabla ya mkutano wao wa ana kwa ana katika mji mkuu wa Belaruse, Minsk, viongozi hao wawili pia walishiriki katika mazungumzo na afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Ulaya, Catherine Ashton.
Mgogoro nchini Ukraine
Mkutano huo unakuja baada ya askari kumi wa Urusi kukamatwa mashariki mwa Ukraine.
Mwanadiplomasia Ashton ameyaelezea mazungumzo yaliyowashirikia viongozi mbalimbali wa Ulaya kuhusu mgogoro wa Ukraine kuwa una mwelekeo"sahihi".
Umoja wa Ulaya pamoja na Marekani zimeiwekea Urusi vikwazo vya uchumi kwa kushindwa kuwadhibiti waasi. Zaidi ya watu 2,000 wameuawa katika mapigano kati ya majeshi ya Ukraine na waasi katika majimbo ya Donetsk na Luhansk.
Majimbo hayo mawili yamejitangazia uhuru kutoka Kiev kufuatia hatua ya Urusi ya kujinyakulia eneo la kusini la Crimea kutoka Ukraine mwezi March 2014.
Mazungumzo kati ya Bwana Poroshenko na Bwana Putin yalidumu kwa takriban saa mbili bila kuruhusu vyombo vya habari. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Na BBC

WAKUBALIANA KUSITISHA MAPIGANO GAZA


Mashambulio ya Gaza
Usitishaji wa muda mrefu wa mapigano umekubaliwa kati ya Israel na wapiganaji wa Kipalestina katika Ukanda wa Gaza.
Kusitishwa kwa mapigano hayo, kumehitimisha wiki saba za vita vilivyosababisha vifo vya watu zaidi ya 2,200, wengi wao wakiwa Wapalestina. Mazungumzo hayo yalisimamiwa na Misri na yalianza kutekelezwa jana moja usiku.
Hamas wamesema mpango huo unawakilisha "ushindi wa upinzani wao".
Maafisa wa Israel wamesema Israel italegeza vikwazo ilivyoiwekea Gaza ili kuruhusu misaada na vifaa vya ujenzi kuingia Gaza.

Mahmud Abbas kiongozi wa Wapalestina
Rais wa Wapalestina Mahmoud Abbas ametangaza kukubaliana na mpango wa kusitisha mapigano.
Msemaji wa serikali ya Israeli, Mark Regev amesema: "hebu tuwe na matumaini kwamba mpango huu wa kusitisha mapigano utaheshimika"
Mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja katika masuala yenye utata, ikiwa ni pamoja na wito wa Israel wa kuyataka makundi ya wapiganaji yanapokonywa silaha, yataanza mjini Cairo katika kipindi cha mwezi mmoja. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAN CITY YAIBANA LIVERPOOL 3 - 1


Manchester City yailaza Liverpool 3-0
Mabingwa wa ligi kuu ya Uingereza walifungua kampeini ya kutetea taji lake kwa kuinyuka washindi wa pili msimu uliopita Liverpool mabao 3-1 katika uwanja wao wa nyumbani Etihad.
Stevan Jovetic alipeleka kilio kwa Liverpool kwa kutikisa wavu mara mbili katika kila nusu.
Liverpool ambayo ilijitahidi kucheza vizuri katika kipindi cha kwanza cha mchezo ilishindwa kutumia vizuri fursa ilizopata haswa katika kipindi cha kwanza ilipobainika itambidi Kocha Brendan Rodgers kutafuta mshambulizi mbadala baada ya kumuuza Luis Suarez.
Hata hivyo Rodgers atakuwa akitafuta ufufuo baada ya kumsajili mshambulizi wa Italia Mario Balotelli kwa pauni milioni 16 .
Uwanjani matumaini ya Liverpool kunusurika kichapo yaliambulia patupu , Sergio Aguero sekunde 23 baada ya kuchukua pahala pake Edin Dzeko.
Ushindi huo ni wa pili kwa kwa Man City msimu huu
Liverpool ilipata bao la kufutia machozi baada ya Pablo Zabaleta kujifunga mwenyewe katika dakika 20 za mwisho .
Liverpool itakumbuka Jovetic alipowahangaisha alipokuwa Fiorentina kwa ni jana ndiye aliyekuwa mwiba kwa safu yao ya ulinzi.
Meneja wa Manchester City, Manuela Pellegrini amesema kikosi chake kilionyesha mchezo mzuri ambapo matunda yake ni mabao matatu dhidi ya Liverpool.
Pellegrini anasema ni muhimu kujizolea pointi sita kutoka kwenye michezo miwili ingawa mwanzo ulikua mgumu kwao.
Kwa upande wake Rodgers atajiliwaza na hali ya kuwa wamewasajili wachezaji wapya 9 msimu huu kwa hivyo bado anakisuka kikosi chake kwa niya ya kutetea nafasi yao ya pili ama hata kuiboresha nafasi hiyo ya msimu uliopita.Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...