KUMEKUCHA! Baada ya kuwepo kwa misuguano ya chini kwa chini kati ya viongozi na wanachama wa kundi la waigizaji wa filamu la Bongo Movie Unity, sasa siri imefichuka kuwa baadhi ya watu wanaotajwa kuwania kuteuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) ili wagombee urais mwakani, ndiyo wanaolibomoa kundi hilo kutokana na fedha wanazodaiwa kuzitoa.
Mwenyekiti wa Bongo Muvi, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’.
Baadhi ya waigizaji wenye ushawishi katika kundi hilo waliliambia gazeti hili juzi kwamba, dhambi kubwa inayolitafuna kundi hilo ni kambi za kisiasa zinazoratibiwa na makada wawili wanaoonekana kuwa na ushawishi ndani ya CCM ambao wanatajwa kutaka kumrithi Rais Jakaya Kikwete.
“Unajua
hapa Bongo Muvi kuna watu wamejikita moja kwa moja katika hizi kambi
ambazo kuna waheshimiwa hawa wawili (majina tunayo) ndiyo sababu kuu ya
watu wengine kufikia kujiuzulu kwa hoja kuwa wanatumika kwa manufaa ya
mtu,” alisema mmoja wao aliyeomba hifadhi ya jina lake. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Inadaiwa
kuwa waheshimiwa hao wawili wamekuwa wakitoa fedha ili kufadhili hafla
mbalimbali zinazowahusu waigizaji hao kwa lengo la kutaka kuwatumia muda
rasmi wa kampeni utakapowadia.
“Hata
hizi hafla zinabuniwa na kuratibiwa na wakubwa hao ambao hutoa fedha za
kutosha kwa ajili ya kuzifanikisha. Mfano, kujiuzulu kwa Katibu wa Bongo
Muvi, Mtitu (William) kulitokana na kuyeyuka kwa fungu lililotoka kwa…
(anataja jina).
“Sasa
Mtitu akaona huu ubabaishaji, watu wengine wanufaike wao watumike tu,”
alisema mtoa habari huyo.Akizungumzia hitima ya kuwaombea wasanii wa
filamu waliotangulia mbele ya haki iliyofanyika hivi karibuni katika
Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam ambako Mwenyekiti wa Jumuiya
ya Wazazi Taifa (CCM) Abdallah Bulembo alikuwa mgeni rasmi, mtoa habari
hii alisema kuna ‘fungu’ lilitoka.
Katibu wa
Bongo Muvi aliyejiuzulu, Mtitu aliliambia gazeti hili kuwa ni kweli
amechukua hatua hiyo baada ya kubaini kuwa wanatumika kisiasa kwa faida
ya watu wengine.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Five Effects, William J. Mtitu.
“Nimechoka
kutumiwa kisiasa bila ridhaa yangu, kisingizio Bongo Muvi, kama kuna
mtu au chama kinataka kututumia wasanii au kuitumia Bongo Muvi basi kuwe
na uwazi na siyo kumtumia mtu mmoja kwa manufaa yake mwenyewe,”
alisema.
Mwenyekiti
wa Bongo Muvi, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ alipoulizwa kuhusu ishu
hiyo, alikiri kuzisikia siku nyingi, tokea alipoandaa chakula cha usiku
kwa wadau wake katika Hoteli ya Great Wall iliyopo Masaki jijini Dar.
“Unajua
si kila kitu ni siasa na yote haya yanasemwa kwa kuwa mimi niko kambi ya
huyo mheshimiwa. Kwa vile likitokea jambo lolote Bongo Muvi mi huwa
naenda kwake kuomba msaada.
“Halafu
hakuna mwana Bongo Muvi asiyejua kuwa akaunti yetu ipo tupu, sasa
nikienda kuomba fedha naambiwa niko kambi yake, hilo halina ukweli
wowote,” alisema Steve anayehisiwa kuwa kambi hiyo.
Akikanusha
madai ya kutafuna shilingi milioni 22 kati ya hizo, saba zikiwa ni
malipo waliyochukua kwa ushiriki wao katika tamasha moja na zilizobaki
zikiwa ni michango kutoka kwa matajiri mbalimbali, Steve alisema:
“Ilitoka
shilingi milioni saba kwa ajili ya tamasha, huyo Mtitu ni mmoja wa watu
waliokula zile fedha lakini hazungumzi chochote.
Kuhusu
kupewa milioni kumi na tano na huyo mheshimiwa ili nifanye dua pale
Karimjee Hall si kweli, kuna watu kibao wametoa misaada yao na uzuri
zaidi hakuna aliyetoa fedha taslimu zaidi ya kusema mimi nitafanya kitu
fulani na wamefanya, mimi namsihi Mtitu awe mkweli tu katika hili
asituchonganishe.”
Makada wa
CCM wanaotajwa kuwania nafasi ya kuteuliwa kupeperusha bendera ya chama
hicho 2015 ni Edward Ngoyai Lowassa, Frederick Tuluway Sumaye, Steven
Masatu Wassira, January Yusuf Makamba, Bernard Camillius Membe, Wiliam
Mganga Ngeleja, Samuel John Sitta na hivi karibuni Mizengo Peter Pinda. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Chanzo GPL
No comments:
Post a Comment