(Nje ya bunge la Kenya. Picha na Maktaba)
Bunge la taifa nchini Kenya linapanga kujadili sheria ya kipekee inayopendekezakupigwa mawe hadi kufa kwa raia wa kigeni atayeshiriki mapenzi ya jinsia moja huku wazawa wakikuhukumiwa kifungo cha maisha jela.
Mwandishi na mdhamini wa sheria hiyo Edward Onwong’a Nyakeriga
anapendekeza kuharamishwa kwa ulawiti na kisha kuhukumiwa jela kwa wale wanaotenda
kosa hilo huku akisisitiza kuwa upo
umuhimu wa kuwalinda watoto na vijana ambao wanalengwa na dhulma ambazo
kwa mda mrefu zinaepukwa kutokana na mabadiliko ya teknolojia na habari
isiyo chujwa na watoto yatima kukosa mwakilishi pamoja na majaribio ya
wanaoshiriki uhusiano wa jinsia moja kuwalea watoto ilihali
wanaendeleza uhusiano wao’
Muswada huo wa chama cha Republican Liberty Party unaharamisha
uhusiano wowote wa jinsia moja na tayari umeungwa mkono na wabunge zaidi ya 78 na
wengine zaidi wanaendelea kushawishiwa. Pia spika wa Bunge Mh. Justin Muturi ameupokea na kuuwasilisha katika kamati ya sheria bungeni
ambayo inatathmini kisha kutoa ripoti kwa bunge.
Mmoja kati ya waaandishi wa vitabu maarufu nchini Kenya Binyavanga Wainaina amekua
miongoni mwa waliojitokeza hadharani na kukiri kushiriki mapenzi ya
jinsia moja na wakati huohuo Mashirika ya kutetea haki za wanaoshiriki
mapenzi ya jinsia moja hivi karibuni yaliwasilisha pendekezo la kutaka
Wabunge kuondoa sheria zote zinazowazuia kuishi maisha yao kama watu
wengine. Muswada huo unatarajiwa kupata upinzani mkali kutoka kwa wanaotetea haki
za binadamu.
Kwa upande wa Katiba ya Kenya ya mwaka 2010 imeharamisha ndoa ya jinsia moja japo
haiharamishi moja kwa moja uhusiano wa mapenzi ya jinsia moja ambapo pia
mwezi uliopita utafiti uliofanywa na kampuni ya Ipsos Synovate
umeonyesha kwamba 64% ya Wakenya wanaamini kwamba hisia za kushiriki
mapenzi na jinsia sawa ni jambo la kujifunza ilihali 14% kati yao
wanaamini watu hao huzaliwa walivyo.
Chanzo: Millard Ayo