Siku moja baada
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema kueleza kuwa hakuna
mwenye mamlaka kisheria kuvunja au kusitiza Bunge la Katiba, mwenyekiti
wa Chama cha NCCR-Mageuzi amesema kauli hiyo imejaa unafiki na kwamba
upo uwezekano wa kuahirisha vikao kwa muda mpaka mwafaka wa kitaifa
utakapopatikana.
Mwenyekiti huyo, James Mbatia amesema kuahirisha
Bunge kunawezekana kama ambavyo iliwezekana kusitishwa vikao vya Bunge
hilo Aprili mwaka huu kupisha Bunge la Bajeti na kubadilishwa kwa Sheria
ya Mabadiliko ya Katiba kinyemela kwa kuongeza idadi ya siku za Bunge
la Katiba kutoka 70 hadi 90 mpaka kuwa muda wowote ambao utaonekana
unafaa.
Wakati Mbatia akieleza hayo, jana waliibuka wazee
wa Jiji la Dar es Salaam wakiwataka Watanzania kuyaombea makundi
yanayovutana na moja likisusia vikao vya Bunge hilo vinavyoendelea mjini
Dodoma, ili yakutane na yakubali kufikia mwafaka kwa pamoja.
Kauli ya Mbatia
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar
es Salaam, Mbatia alisema kauli iliyotolewa juzi na Jaji Frederick
Werema imejaa unafiki. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Katika mkutano huo ambao Mbatia pia alieleza
maazimio ya mkutano wa halmashauri kuu ya chama hicho uliofanyika Agosti
14, mwaka huu, alihoji kama Bunge la Katiba haliwezi kusitishwa,
iliwezekana vipi kulisitisha kupisha Bunge la Bajeti.
Mbatia alisema ni jambo la ajabu kuona watu
wakitunga sheria kwa ajili ya kukinufaisha kikundi cha watu wachache na
akasisitiza kuwa kufanya hivyo ni sawa na kuwahadaa Watanzania.
“Kama katika awamu ya kwanza tuliweza kuliahirisha
Bunge la Katiba kupisha Bunge la Bajeti bila kuwapo kwa sheria, pia
tunaweza kulihairisha katika awamu ya pili ya Bunge hilo kupisha
maridhiano. Mshikamao wa kitaifa ni zaidi ya Bunge la Bajeti na kitu
chochote,” alisema.
“Tatizo la Watanzania ni kuwa na umaskini wa fikra
uliobebwa na ujinga, fitna, umbeya, kusema uongo, kujenga chuki katika
jamii na uvivu wa kufikiri. Maridhiano ya kitaifa ni njia pekee ya
kunusuru mchakato wa Katiba.”
Alisema wajumbe wanaoendelea na vikao vya Bunge
hilo mjini Dodoma wanakusudia kupitisha rasimu kwa ajili ya kukibeba
chama kimoja cha siasa na siyo kwa ajili ya masilahi wa Watanzania.
“Dola inaundwa kwa msingi wa maridhiano, siasa
inafuata baadaye. Hilo lilifanyika Zanzibar na nchi nyingi barani Afrika
zilizokumbwa na machafuko ya wenyewe kwa wenyewe wakati wa kuandika
Katiba,” alisisitiza.
Akizungumzia maazimio ya halmashauri kuu, Mbatia
alisema: “Tumeitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuliweka hadharani Daftari
la Kudumu la Wapigakura lililoboreshwa mwaka 2010, kutokana na hivi
karibuni tume hiyo kueleza kuwa hakuna daftari. Tunajiuliza kama halipo
hata walioshinda chaguzi zilizopita siyo halali.”
Na Mwananchi
Alisema kwa kauli hiyo maana yake ni kwamba ukifanyika uchaguzi
wowote nchini hakuna atakayeweza kupiga kura, kutaka mfumo wa
uandikishaji wapigakura wa kieletroniki (BVR) uwekwe wazi na kusimamiwa
na Tume Huru ya Uchaguzi yenye weledi, kutokana na kukiri hadharani kuwa
iliyopo sasa imeshindwa kazi.
“Tunaitaka Serikali itamke wazi tarehe ya Uchaguzi
wa Serikali za Mitaa na usimamiwe na Tume Huru ya Uchaguzi kwa kutumia
Daftari la Kudumu la Wapigakura lililoboreshwa,” alisisitiza.
Wazee wa Dar es Salaam
Wakati huohuo, wazee watano wa Dar es Salaam Yahya
Ngoma, Kapteni mstaafu, Alhaji Mohammed Ligora, Ali Bakari Mukhi na
Alhaji Omari Chiwaka wamewataka Watanzania kuyaombea makundi
yanayovutana katika mchakato wa Katiba.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake katika Ukumbi wa
Idara ya Habari Maelezo, Alhaji Ligora alisema kitendo cha Umoja wa
Katiba ya Wananchi (Ukawa) kususia vikao vya Bunge hilo na wenzao
wakiendelea na vikao kinatakiwa kuombewa.
“Hakuna haja ya kuwazomea hawa na kuwafurahia wale
au kinyume chake. Tunatakiwa kuwaombea ni shetani tu kaingia kati yao,”
alisema Alhaji Ligora. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz
Na Mwananchi
No comments:
Post a Comment