Sunday, March 18, 2018

RAIS MWANAMKE PEKEE AFRIKA AJIUZULU

Rais wa Mauritius, Ameenah Gurib-Fakim.

AMEENAH Gurib-Fakim rais wa Mauritius amejiuzulu urais baada ya kuelekezewa tuhuma za ufisadi kwa kutumia kadi ya malipo; awali alisema hatajiuzulu.
Baada ya kung’atuka madarakani kwa rais Sirleaf Johnson wa Liberia, huyu ndiye alikuwa mhimili wa wanawake Afrika kujishikilia kwa kusema "tuna Rais mwanamke" lakini sasa madai ya ufisadi yanaelekea kumtega.
Amehusishwa na kashfa ya kutumia kadi ya benki ambayo alikuwa amekabidhiwa na wahisani ya kufadhili ununuzi wa misaada kwa raia wake kujifaa yeye mwenyewe.
Kitita alichokigeuza kuwa chake ndani ya kadi hiyo kinasemwa kuwa makumi ya maelfu ya dola za Kimarekani.
Alijitetea kuwa hakufanya lolote baya na kwamba amerejesha pesa ambazo amedaiwa kujifaa nazo, hivyo basi kuweka swali wazi kuhusu "utarejesha nini ikiwa hukuiba".

Gurib-Fakim akiwa ni mwanasayansi tajika, alipaa hadi uongozi wa Mauritius mwaka wa 2015, ingawa ni wadhifa ambao hauna mamlaka yale ya viongozi wengine wa AfrikaTunapenda kuwataarifu wadau wetu kuwa hivi karibuni tutapatikana kwa website ya jambotz.co.tz

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI MARCH 18, 2018 YA DINI, MICHEZO NA HARD NEWS



Tunapenda kuwataarifu wadau wetu kuwa hivi karibuni tutapatikana kwa website ya jambotz.co.tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...