Watoa
huduma za uokoaji huko mji mkuu wa Nepal Kathmandu, wamefanikiwa
kumuokoa kijana mmoja mwenye umri wa miaka 15 aliyepatikana hai baada ya
funikwa na vifusi vya jengo alilokuwemo wakati wa tetemeko la ardhi
kukumba taifa hilo siku tano zilizopita.
Licha ya kuwa chini ya
maporomoko hayo kwa siku hizo tano isaidiwa na mwanya uliokuwa
ukipenyeza hewa iliyomwezesha kupumua japo kwa shida. Makundi ya
watu walimshangilia alipotolewa huku akionekana akijitahidi kufungua
macho yake.Alikimbizwa hospitali mara moja kupata matibabu zaidi.
Zaidi ya watu 5,500 wamethibitishwa kufariki kutokana na janga hilo. Wengi
wa wanavijiji wangali wanasubiri misaada ya chakula na maji safi ya
kunywa huku mashirika ya kutoa misaada ya kisema huenda ikachukua siku
nyengine 5 kabla ya kuwafikia baadhi yao kutokana na kuharibiwa kabisa
kwa miundo mbinu.
Umoja wa mataifa umetoa wito kwa jumuiya ya
kimataifa kuendelea kutoa misaada wakikadiria michango inayohitajika
kuwa zaidi ya dolla millioni 415 kuisaidia Nepal katika kipindi cha
miezi 3 ijayo. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.
No comments:
Post a Comment