SERIKALI imetoa kauli kuhusu tuhuma
zilizokuwa zikiwakabili baadhi ya mawaziri, waliobatizwa jina la
‘Mawaziri Mizigo’, na hatua ambazo zimekuwa zikichukuliwa kukabiliana na
kero zilizosababisha wapewe jina hilo. Akizungumza
na waandishi wa habari jana Ikulu Dar es Salaam, Katibu Mkuu Kiongozi,
Balozi Ombeni Safue, alisema mawaziri hao walituhumiwa kutokana na
changamoto zilizopo katika wizara zao; na si upungufu wao binafsi kama
viongozi.
Mawaziri hao saba walitajwa katika ziara ya mikoani ya
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na baadae walihojiwa katika
kikao cha Kamati Kuu cha chama hicho.
Baada ya kuhojiwa, Katibu
wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alisema
Kamati Kuu ilimuachia Rais Kikwete jukumu la kuamua kuwafukuza kazi,
kuwahamisha au kuwataka kutekeleza majukumu yao kikamilifu.
Miongoni mwa mawaziri waliohojiwa ni aliyekuwa Naibu Waziri wa Fedha, Saada Mkuya, ambaye sasa ameteuliwa kuwa Waziri wa Fedha.
Kwanza: Matumizi yake; meno ya tembo hutumika kutengeneza vitu vya
urembo kama vile hereni , mikufu, mapambo kama vile sanamu na hata keys
za keyboards za vinanda. Vifaa vilivyotengenezwa kwa meno ya tembo hutumika nchini China kama sehemu ya kuonyesha ufahari, kwa mujibu wa Wikipedia.
Pili: Bei ya meno ya tembo Bei inategemea na soko , hata hivyo kwa mujibu wa answers.com , jino moja la tembo huweza kuuzwa kwa dola za kimarekani mia saba (700).