Wednesday, September 04, 2013

WAZAZI WATELEKEZA WATOTO HOTELINI KWA MIEZI MITATU, WADAIWA MILIONI 3

Na Steven Kanyeph - SHINYANGA 
Wazazi ambao hawajulikani makazi yao maalumu wameitelekeza familia ya watoto wao wanne katika hoteli ya Ibanza iliyopo mjini Shinyanga kwa takribani miezi 3 ambapo mpaka sasa wanadaiwa kiasi cha shilingi milioni tatu. 

Mhasibu wa Hoteli hiyo bwana Julius Kiungu amemtaja bi Christina Peter ambaye ni mzazi wa watoto hao kuwa alifika katika hoteli ya Ibanza Mei, 15 mwaka huu akiwa na watoto wa wanne kwa lengo la kupumzika. Bi Chritina ambaye ni mzazi wa watoto hao alieendelea kuwepo katika hoteli hiyo kwa takribani wiki mbili lakini baada ya hapo aliondoka bila taarifa na kuwatelekeza watoto wake katika hoteli hiyo. Tembelea http://jambotz8.blogspot.com/ kila siku.

Mmoja wa watoto hao aliyejitambulisha kwa jina la Teddy Masumbuko mwenye umri wa miaka 20 amesema kuwa anashangazwa na kitendo cha mama yao kuondoka bila kutoa taarifa huku akimuacha na wadogo zake watatu wenye umri mdogo. Msemaji wa hoteli hiyo bwana Julius Kiungu anawaomba ndugu, jamaa na marafiki wa familia hiyo wafike ili kuwachukuwa watoto hao kwa ulinzi na usalama wa watoto hao.

MWANAMKE AKAMATWA NA DAWA ZA KULEVYA UWANJA WA NDEGE JNIA LEO MCHANA JIJINI DAR ES SALAAM TANZANIA

Jitihada za kurejesha heshima kwa viwanja vya ndege nchini zilizoanzishwa na waziri wa uchukuzu Dk. Harisson Mwakyembe zinaonekana kuzaa matunda baada ya mwanadada kutoka nchini Nigeria Anthonia Ojo (25) kukamatwa na kete 99 za madawa ya kulevya Dar es Salaam leo.

Zifuatazo ni picha mbalimbali za tukio zima la kunaswa kwa mtuhumiwa huyo ambapo anashikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi wakati kete hizo zimepelekwa kwa ofisi ya Mkemia Mkuu kwa uchunguzi zaidi. 

ANTHONIA OJO AKIWASILI KITUO CHA POLISI CHA JNIA BAADA KUKAMATWA.
ANTHONIA OJO AKIELEKEA KWENYE GARI BAADA YA KUKAMATWA

MAGAZETI YA LEO JUMATANO SEPTEMBA 04, 2013

DSC 0018 857f5
DSC 0019 bd620

WAJUA KWANINI UNAHITAJI KULALA?

kulala_39d75.jpg
Wanasayansi wanaamini kuwa wamepata sababu moja mpya ya kwa nini tunahitaji usingizi.
Wanasema kuwa kulala kunasaidia katika kujenga celi mpya za ubongo.

Usingizi unasaidia kuzalisha upya celi za ubongo ambazo nazo hujenga kemikali inayojulikana kama Myelin ambayo ni muhimu katika kulinda ubongo wetu kwa ambavyo unafanya kazi.


Matokeo ya utafiti huu ambayo yalijitokeza katika panya wa mahabara, huenda yakachochea maelezo zaidi kuhusu umuhimu wa usingizi katika kukabarabati celi za ubongo na kukuza celi mpya pamoja na kuulinda kutokana na magonjwa.

Daktari Chiara Cirelli na wenzake kutoka chuo kikuu cha Wisconsin waligundua kuwa Panya hao walipokuwa wanalala, ndipo kemilaki hiyo ilikuwa inatengezwa kwa wingi na celi za mwili.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...