Monday, October 05, 2015

RAIS KIKWETE ATEUA WAKUU WA WILAYA 13





Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete
Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete 

Rais Jakaya Kikwete amewateua wakuu wapya 13 wa wilaya na kuwahamisha vituo vya kazi wengine saba.
Walioteuliwa ni Shaaban Ntanambe ambaye anakwenda Chato; Thabisa Mwalapwa (Hanang), Richard Kasesera (Iringa), Ruth Msafiri (Kibondo) na Abdallah Njwayo (Kilwa).

Wengine ni Asumpta Mshama (Wanging’ombe), Mohammed Utaly (Mpwapwa), Dauda Yasin (Makete), Honorata Chitanda (Ngara), Vita Kawawa (Kahama), Christopher Ng’ubyagai (Mkalama), Hawa Ng’humbi (Kishapu) na Mrisho Gambo (Uvinza).

Wakuu wa wilaya waliohamishwa vituo vya kazi ni Fadhili Nkurlu ambaye anatoka Mkalama, kwenda Wilaya ya Arusha, Wilson Nkambaku anahamishiwa Arumeru, kutoka Kishapu, Francis Miti ambaye anahama Hanang kwenda Monduli na Jowika Kasunga ambaye anahamia Mufindi kutoka Monduli.

Wengine waliohamishwa ni Muhingo Rweyemamu kutoka Makete kwenda Morogoro; Hadija Nyembo anayehamia Kaliua kutoka Uvinza na Benson Mpesya ambaye anahamia Songea Ruvuma kutoka Kahama. Asante kwa kutembelea blog yetu, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kulike page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.

DEREVA BODABODA AUAWA NA KUNYOFOLEWA KICHWA NA SEHEMU ZA SIRI



 Waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda wakiwa katika kijiwe chao. PICHA NA MAKTABA

Watu wasiofahamika wamemuua kwa kumchinja mwendesha pikipiki maarufu kama bodaboda, Hosam Abdallahaman (18) na kutoweka na kichwa chake, sehemu zake za siri na pikipiki.   

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Hamis Issa alithibitisha kutokea kwa mauaji hayo juzi usiku katika Kijiji cha Silimka, Kata ya Itilo wilayani hapa.



Kamanda Issa alisema kabla ya mauaji hayo, saa moja usiku, Hosam alikodiwa na abiria ampeleke eneo la Silimka na hakurudi kwenye kituo chake cha kazi hadi alipokutwa akiwa ameuawa majira ya saa 4 asubuhi siku iliyofuata. Asante kwa kutembelea blog yetu, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kulike page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.

KIKWETE NA UHURU WAZINDUA BARABARA MUHIMU

Barabara hiyo ni ya pili kufadhiliwa na AfDB baada ya ile ya Arusha-Namanga / Namanga - Athi River
 
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na mwenzake wa Tanzania Jakaya Kikwete wamezindua mradi wa ujenzi wa barabara ya Taveta-Mwatate ambayo inatarajiwa kurahisisha uchukuzi kati ya kataifa hayo mawili.

Barabara ya Arusha-Holili upande wa Tanzania pia inakarabatiwa. Rais Kikwete yumo nchini Kenya kwa ziara rasmi ya siku tatu na Jumanne anatarajiwa kuhutubia kikao cha pamoja cha mabunge mawili ya Kenya.

Mradi wa ujenzi wa barabara hizo mbili umefadhiliwa kwa pamoja na Benki ya Maendeleo ya Afrika na serikali za Kenya na Tanzania. Asante kwa kutembelea blog yetu, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kulike page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.

WENGER AFURAHIA USHINDI DHIDI YA MAN UTD

Arsene Wenger
 
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger ameeleza furaha yake baada ya klabu hiyo kupata ushindi wa 3-0 dhidi ya mahasimu wao wa jadi Manchester United katika Ligi Kuu ya Uingereza Jumapili.

Wenger amesema alifurahishwa sana na uchezaji wa timu yake na kueleza kuwa walishangaza Manchester United kuanzia mwanzo wa mechi.

“Kuanzia kwa Petr Cech hadi kwa Theo Walcott wote walicheza vyema. Nimenoa timu nyingi kali lakini hakuna hata moja iliyoweza kucheza mechi 60 katika kiwango sawa. Lazima ukubali kwamba sisi ni binadamu,” alisema.

“Tuko kwenye kinyang’anyiro (cha kushindania taji), tuko alama mbili nyuma ya viongozi Manchester City na natumai matokeo ya leo yatatupa imani ya kuendelea kupigania taji.” Asante kwa kutembelea blog yetu, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kulike page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.

TP MAZEMBE KUKUTANA NA ALGER FAINALI

Timu ya TP Mazembe 
 
Klabu ya TP Mazembe ya Congo DRC, Itakutana na klabu ya Algeria USM Alger katika hatua ya fainali ya klabu bingwa barani Afrika.

Mazembe ilijihakikishia nafasi yake siku ya jumapili yaani jana baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya El Merrekh ya Sudan mjini Lubumbashi.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta alifunga mara mbili katika ushindi huo huku Muivarycoast Roger Assale akifunga goli la tatu. Asante kwa kutembelea blog yetu, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kulike page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.

SOMA MAGAZETI YA LEO JUMATATU OKTOBA 05, YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

.
.
.
Asante kwa kutembelea blog yetu, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kulike page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...