Rais wa Kenya Uhuru
Kenyatta na mwenzake wa Tanzania Jakaya Kikwete wamezindua mradi wa
ujenzi wa barabara ya Taveta-Mwatate ambayo inatarajiwa kurahisisha
uchukuzi kati ya kataifa hayo mawili.
Barabara ya Arusha-Holili upande wa Tanzania pia inakarabatiwa. Rais
Kikwete yumo nchini Kenya kwa ziara rasmi ya siku tatu na Jumanne
anatarajiwa kuhutubia kikao cha pamoja cha mabunge mawili ya Kenya.
Mradi wa ujenzi wa barabara hizo mbili umefadhiliwa kwa pamoja na Benki ya Maendeleo ya Afrika na serikali za Kenya na Tanzania. Asante kwa kutembelea blog yetu, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kulike page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.
Kwa
mujibu wa mkurugenzi wa kanda hii wa AfDB Gabriel Negatu benki hiyo
imetoa $218 milioni za kutumiwa kwenye mradi huo, Kenya ikipokea $116
milioni na Tanzania $102 milioni.
Huo ndio mradi wa pili wa
barabara wa kuunganisha Kenya na Tanzania uliofadhiliwa na benki hiyo,
wa kwanza ukiwa barabara za Arusha-Namanga/Namanga-Athi River.
Rais
Kikwete alisema barabara hiyo ya Taveta-Mwatate hutumiwa na wakazi wa
kaskazini na kaskazini-magharibi mwa Tanzania kusafirisha bidhaa hadi
Mombasa.
“Huchukua saa 14 kutoka Arusha hadi Voi. Lakini ujenzi
huu ukikamilika, itachukua saa mbili na nusu pekee, hivyo kuwa nafuu
sana kwa wasafiri na wenye magari,” alisema.
Kiongozi huyo,
anayetarajiwa kuondoka mamlakani karibuni baada ya uchaguzi mkuu Oktoba
25, alisema barabara hiyo ina uwezo wa kuimarisha biashara kati ya Kenya
na Tanzania kwa asilimia 10. Asante kwa kutembelea blog yetu, kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa kulike page yetu ya facebook bofya neno Jambo Tz.
No comments:
Post a Comment