Saturday, February 15, 2014

MBEYA CITY YATOKA SARE NA SIMBA, YANGA YAINYUKA TENA KOMOROZINE

goal 
Mchezo uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu baina ya vilabu vya Simba na Mbeya City uliokuwa unachezwa leo huko jijini Mbeya katika dimba la Sokoine umemalizika.
Matokeo ya mchezo huo ni sare ya bao moja kwa moja, Mbeya City ndio walioanza kuliona lango la Simba katika dakika ya 17 kwa mkwaju wa penati, bao hilo lilidumu mpaka mapumziko wenyeji wakitoka kifua mbele.
simba-mpya-2 
Kipindi cha pili Simba walianza kwa kasi na hatimaye katika dakika ya 50, mshambuliaji hatari wa Simba Mrundi Amiss Tambwe akaifungia timu yake bao la kusawazisha.
Timu hizo ziliendelea kushambuliana lakini mpaka refa anapuliza kipenga cha mwisho matokeo yalibaki moja kwa Mbeya City na moja kwa Simba. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz  

KUTOKA COMORO
DSC_0051 
Mabingwa wa Tanzania bara na wawakilishi wa nchi katika michuano ya kombe la mabingwa wa Afrika Dar Young African imefanikiwa kuvuka kwenda raundi ya pili ya michuano hiyo baada ya kuifunga timu ya Komorozine De Domoni mabao 5-2.
Mabao ya Yanga yamefungwa na Mrisho Ngassa aliyefunga hat trick, huku Hamis Kiiza na Msuva wakifunga bao moja moja.
Yanga sasa watakutana na timu kubwa ya Misri Naciona Al Ahly.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz  

HIKI NDICHO ALICHOANDIKA KALA JEREMIAH KUHUSU AJALI ALIYOPATA SIKU YA VALENTINE

kala-ajali  
Leo Kala Jeremiah kupitia ukurasa wake wa Instagram amepost picha inayoonyesha ajali aliyoipata wakati akitokea kwenye show yake iliyokuwa ikifanyika Club East 24 ambayo alikua akifanya show pamoja The B Band ya Banana Zoro.
kala 
Hiki ndicho alichokipost Kala Jeremiah kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Screenshot_2014-02-15-14-35-32 
Chini ya Post ya picha ya gari yake Kala aliandika maneno haya>> nIMEPATA AJALI USIKU HUU NIKIWA NATOKEA CLUB EAST 24 AMBAKO NILIKUWA NAFANYA SHOW NA B BAND WAKATI NARUDI NYUMBANI GHAFLA KUNA MTU WA PIKIPIKI AKAWA ANATAKA KUINGIA NIKAJARIBU KUMKWEPA GARI ILIKUA MWENDO KASI KIDOGO IKAYUMBA KWENDA KULIA NIKAIRUDISHA IKARUDI ZAIDI KUSHOTO NIKAIRUDISHA TENA KULIA IKAWA INATAKA KWENDA MTARONI NIKAIRUDISHA TENA KUSHOTO AMBAKO ILIGEUKA ILIKUKUA INATOKA NA KUINGIA MTARONI AMBAKO ILIKITA NA KUVUNJA MLANGO WA UPANDE WANGU.SIJAAMINI KAMA NIMETOKA BILA HATA JERAHA MGUUNI WALA MAUMIVU ZAIDI YA YALE UA KICHWANI KIDOGO NILIYOJIGONGEA KWENYE MLANGO KWA JUU.AHSANTE SANA MUNGU UMENIOKOA.ASANTE SANA MUNGU WANGU.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz  

AL-SHABAAB WAPATA SILAHA ZA SERIKALI...!!!

Ripoti ya umoja wa mataifa imeonya kuwa silaha zilizokuwa zikipelekwa kwa vikosi vya serikali ya Somali zimeingia katika mikono ya kundi la Al-shabaab kutokana na ukiukwaji wa utaratibu katika serikali.
Uchunguzi huo uliofanywa na wataalam walio huru umesema kuwa silaha za kudungua ndege,mabomu na risasi zilizotoka nchini Uganda na Djibout haziwezi kuwajibikiwa.
Ripoti hiyo sasa inataka taifa la Somali kuwekewa vikwazo vya silaha ambavyo viliondolewa mwaka uliopita.
Wataalam hao wamesema kuwa wana ushahidi kwamba mshauri mkuu wa rais nchini Somali amekuwa akihusika na mpango wa kuwapelekea silaha wapiganaji wa Alshabaab. 
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI FEBRUARI 15, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS



.. 

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz


YANGA KUSHUKA DIMBANI NA COMORO LEO



WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Yanga leo inatarajiwa kushuka dimbani ikiwa ughaibuni kwa kuumana na Komorozine ya Comoro katika pambano la marudiano la michuano hiyo.
Mechi hiyo inatarajiwa kuchezwa kwenye uwanja wa Sheikh Said Mohamed International uliopo mji wa Mitsamihuli na Yanga ina kazi nyepesi ya kukamilisha ushindi mnono iliyopata katika mechi yao ya nyumbani ilipoisasambua Komorozine mabao 7-0.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Comoro zilizoripotiwa na mtandao wa klabu hiyo ni kwamba mara baada ya juzi jioni kufanya mazoezi mepesi katika uwanja mdogo wa hotel ya Retaj, Yanga ilijifua tena jana  asubuhi majira ya saa 5 ausbuhi katika Uwanja wa Sheikh Said kwa ajili ya kuuzoea tayari kwa ajili ya mchezo wa leo.
Kocha mkuu wa Young Africans Hans Van der Pluijm amesema anashukuru kikosi chake kipo vizuri kuelekea mchezo huo na hakuna mchezaji majeruhi hata mmoja hivyo anapata fursa ya kuchagua amtumie nani katika mchezo huo.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz 

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...