Mchezo uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu baina ya vilabu vya Simba na Mbeya City uliokuwa unachezwa leo huko jijini Mbeya katika dimba la Sokoine umemalizika.
Matokeo ya mchezo huo ni sare ya bao moja kwa moja, Mbeya City ndio walioanza kuliona lango la Simba katika dakika ya 17 kwa mkwaju wa penati, bao hilo lilidumu mpaka mapumziko wenyeji wakitoka kifua mbele.
Kipindi cha pili Simba walianza kwa kasi na hatimaye katika dakika ya 50, mshambuliaji hatari wa Simba Mrundi Amiss Tambwe akaifungia timu yake bao la kusawazisha.
Timu hizo ziliendelea kushambuliana lakini mpaka refa anapuliza kipenga cha mwisho matokeo yalibaki moja kwa Mbeya City na moja kwa Simba. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
KUTOKA COMORO
Mabingwa wa Tanzania bara na wawakilishi wa nchi katika michuano ya kombe la mabingwa wa Afrika Dar Young African imefanikiwa kuvuka kwenda raundi ya pili ya michuano hiyo baada ya kuifunga timu ya Komorozine De Domoni mabao 5-2.
Mabao ya Yanga yamefungwa na Mrisho Ngassa aliyefunga hat trick, huku Hamis Kiiza na Msuva wakifunga bao moja moja.
Yanga sasa watakutana na timu kubwa ya Misri Naciona Al Ahly.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
No comments:
Post a Comment