Ripoti ya
umoja wa mataifa imeonya kuwa silaha zilizokuwa zikipelekwa kwa vikosi
vya serikali ya Somali zimeingia katika mikono ya kundi la Al-shabaab
kutokana na ukiukwaji wa utaratibu katika serikali.
Uchunguzi huo uliofanywa na wataalam
walio huru umesema kuwa silaha za kudungua ndege,mabomu na risasi
zilizotoka nchini Uganda na Djibout haziwezi kuwajibikiwa.
Ripoti hiyo sasa inataka taifa la Somali kuwekewa vikwazo vya silaha ambavyo viliondolewa mwaka uliopita.
Wataalam hao wamesema kuwa wana
ushahidi kwamba mshauri mkuu wa rais nchini Somali amekuwa akihusika na
mpango wa kuwapelekea silaha wapiganaji wa Alshabaab.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz
No comments:
Post a Comment