Na Dustan Shekidele, Morogoro
MWANAMKE aliyefahamika kwa jina la
Bahati ambaye ni mke wa Mrisho Juma, hivi karibuni alikumbwa na aibu ya
aina yake baada ya kunaswa laivu ‘akingonoka’ na shemeji yake.
Tukio hilo
lililoshuhudiwa na umati wa watu lilijiri Machi 11, mwaka huu mchana
kweupee katika eneo la Mafisa kwa Mbambi ndani ya chumba cha Mbaji Hamis
ambaye ni mdogo wa Mrisho.
Akizungumza
na mwandishi wetu, Mrisho ambaye anafanya kazi ya kupiga debe katika
stendi ya mabasi ya Msamvu alisema, fumanizi hilo halikutokea kwa kuweka
mtego bali ni Mungu tu.
Alieleza
kuwa alikamatwa Ijumaa na kutupwa mahabusu kwa kosa la kutovaa
‘yunifomu’. Mkewe na mdogo wake wakawa wanampelekea chakula.
“Jumapili
jioni walikuja tena kuniletea chakula ila kwa bahati nzuri Jumatatu
nikapewa onyo na kuachiwa. Cha ajabu nilipofika nyumbani nilimkuta mtoto
wangu wa miaka 2 analelewa na majirani.
“Nilipowauliza mke wangu yuko wapi walidai tangu Jumamosi hajaonekana kwa maelezo kwamba amekwenda kushughulikia dhamana yangu,” alisema Mrisho na kuongeza kuwa aliendelea kumtafuta sehemu mbalimbali hadi alipoamua kwenda nyumbani kwa mdogo wake.
“Nilipofika
nilimkuta mke na mdogo wangu wakiwa pamoja kitandani. Baada ya mdogo
wangu kuniona alinyanyuka na kuvaa bukta kisha akatoka nduki,” alisema
Mrisho.
Ikaelezwa kuwa, baada ya mwanaume
huyo kumfumania mkewe huku majirani wakishuhudia, alimshushia kipigo
kisha akampa talaka kabla ya kuamua kumrudisha kwao Tabora.
Akizungumza
na mwandishi wetu kuhusiana na kufumaniwa huko, Bahati alisema shemeji
yake alimlazimisha kulala naye baada ya kutoka polisi kumpelekea chakula
mumewe.
Mjumbe wa Serikali ya Mtaa, Rehema Dimoso alikiri kutokea kwa tukio hilo kwenye mtaa wake.
No comments:
Post a Comment