Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea barua kutoka uongozi wa Simba
ikielezea kutotambua mkutano ulioandaliwa na wanaodaiwa kuwa wanachama
wake na kufanyika jana ukumbi wa Starlight, Dar es Salaam.
Vilevile
katika barua hiyo uongozi wa Simba umeahidi kuitisha mkutano wa
wanachama wake. Mkutano huo utaitishwa na Mwenyekiti wa Simba kwa mujibu
wa katiba ya klabu hiyo.
Kutokana na
hali hiyo, TFF imeitisha mara moja kikao cha Kamati ya Sheria, Maadili
na Hadhi za Wachezaji kinachoongozwa na Wakili Alex Mgongolwa kwa ajili
ya kutoa mwongozo kwa matukio ya aina hiyo.
Hata hivyo,
TFF tunasisitiza kwa wanachama wetu ikiwemo Simba kuwa wanachama
wanapotaka kufanya uamuzi wowote ule wanatakiwa kuzingatia katiba na
kanuni zilizopo.
No comments:
Post a Comment