Friday, September 06, 2013

RAIS KIKWETE NA KAGAME WAMALIZA TOFAUTI ZAO NA KUKUBALIANA KUSHIRIKIANA KAMA ZAMANI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Alhamisi, Septemba 5, 2013, amekutana kwa faragha na Rais wa Rwanda, Mheshimiwa Paul Kagame katika mazungumzo yaliyokwenda vizuri na kuwaridhisha viongozi hao wawili wa nchi jirani. 
 
Viongozi hao wamekutana kwa zaidi kidogo ya saa moja katika mkutano uliofanyika kwenye Hoteli ya Munyonyo Commonwealth Resort, nje kidogo ya mji wa Kampala, Uganda.
Katika mazungumzo hayo, Rais Kikwete na Rais Kagame wamekubaliana kuendelea kushirikiana katika kujenga uhusiano mzuri na wa kihistoria uliopo kati ya nchi hizo mbili.

MAGAZETI YA LEO IJUMAA SEPTEMBA 06, 2013

DSC 0038 e6e54
DSC 0039 38cfe

GHASIA KUBWA ZALIPUKA BUNGENI KUPINGA MUSWADA.....!!!

vurugusugu_dd67c.jpg
Jana, Bingwa wa Dunia wa uzani wa kati (super middle), unaotambuliwa na Shirikisho la Ngumi Duniani (WBF), Francis Cheka alitembelea Bunge baada ya kutwaa taji hilo karibuni na jana hiyohiyo, Bunge hilo lilishuhudia ngumi kavukavu katika vurugu kubwa pengine kuliko zote zilizowahi kutokea katika ukumbi wake.Katika masumbwi hayo yasiyo rasmi, Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi 'Sugu' anadaiwa kumpiga kichwa Askari wa Bunge na kumchania sare na kung'oa kipaza sauti.
Mbilinyi jana alisema alikuwa anatafutwa na polisi huku akisema hilo limemshangaza akidai kwamba yeye ndiye aliyeshambuliwa na askari huyo.
Vurugu hizo zilitokea baada ya Naibu Spika, Job Ndugai kuamuru kutolewa nje kwa Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe.
Katika vurugu hizo Mbilinyi alibebwa juujuu na polisi hadi nje ya ukumbi huku akiwa hana viatu.
Pamoja na tafrani hiyo, Ndugai alisema wakati akihitimisha kikao cha Bunge kipindi cha asubuhi kuwa amewasamehe wabunge wote waliohusika na kosa hilo la utovu wa nidhamu na kuwaruhusu kurejea kipindi cha jioni kuendelea na Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Hata hivyo, wabunge wote CUF, NCCR-Mageuzi na Chadema ambao baada ya tukio hilo walitoka nje ya ukumbi, hawakurejea na baadaye walitoa msimamo wa pamoja wakisema hawatashiriki katika mjadala huo.

BAADA YA DAYNA, BABA LEVO NAE AFUNGUKA NA KUDAI KUIBIWA KORASI YA WIMBO MPYA WA DIAMOND "MY NUMBER ONE"...!!!

https://fbcdn-sphotos-a-a.akamaihd.net/hphotos-ak-prn2/q83/1185392_659474667396477_477324071_n.jpg
NARUDIA tena nina asilimia 100 DAIMOND PLATNUM amecopy KORAS yangu coz nimekuwa nikimuimbia kila tunapokutana kwa lengo la kumshirikisha kwenye wimbo wangu (SWEATY SWEATY) ni zaidi ya miezi saba au nane imepita akinizungusha tu.
Na kwa kudhibitisha Hilo mimi nina DEMO 5 za KORASI yangu ambazo nimefanya kwenye studio mbali mbali Ya kwanza 1 kwa MORE FIRE magomeni 2 STUDIO SINZA 3 kwa TUDY THOMAS mbezi 4 kwa G BAKUZA KIGOMA 5 kwa MR T TOUCH mwenge... 
Ninaweza kuwasikilizisha watu demo zote Tano lakini sio kuuachia huo wimbo coz ntaonekana walewale wategemea KICK. wakati MIMI KWA SASA sihitaji kick ya mtu coz msimu huu nina nguvu ya kutosha. na nina jiamini.. ukitaka kuamini angalia kilichotokea FIESTA MTWARA JUZI..

MAWAZIRI WATEJA WA MACHANGUDOA WATAJWA.......!!!



BAADHI ya Mawaziri na askari polisi wametajwa kuwa ni wateja wakubwa wa wanawake wanaouza miili yao(Machangudoa).

Hayo yameelezwa na jukwaa la wanaharakati wanawake vijana (YFF), walipokuwa wakiwasilisha ujumbe wao kwa njia ya sanaa ya ngonjera, katika tamasha la 11 la Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP) linaloendelea eneo la Mabibo Jijini Dar es Salam.

"TATIZO LA UJENZI HOLELA NI KUBWA JIJINI DAR" SERIKALI

majengo_234e1.jpg
Serikali imekiri kuwa kumekuwa na ukiukwaji wa ujenzi ambao haufuati kanuni, taratibu na sheria zilizopo hususan katika Jiji la Dar es Salaam.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Hawa Ghasia ambaye alisema kuwa Serikali imeliona jambo hilo na sasa inapitia sheria upya ili kurekebisha hali hiyo.
Waziri aliyataja maeneo ambayo yanahusika na ukiukwaji ni pamoja na utoaji wa vibali vya ujenzi pamoja na ubadirishwaji wa matumizi ya ardhi na uvamizi wa viwanja vya wazi.
Maeneo mengine ni ukiukwaki wa maadili ya kitaaluma usiozingatia sheria ya mwaka 2007 ya sheria ya mipango miji na kanuni za udhibiti wa ujenzi.

Alikuwa akijibu swali la Muhammed Amour Chombo (Magomeni,CCM) aliyetaka kujua Serikali ina mkakati gani wa kukomesha utovu wa nidhamu dhidi ya waliopewa dhamana ya kusimamia sheria za mipango miji katika kuruhusu ujenzi.

CHEKA ATINGA BUNGENI NA UBINGWA WA WBF



Waziri Mkuu Mh, Mizengo Pinda wanne kushoto akiwa na bingwa wa dunia wa mchezo wa masumbwi nchini Fransic Cheka baada ya kukaribishwa bungeni mjini Dodoma wengine kushoto Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D'  na bingwa wa mabara Fransic Miyeyusho kulia ni promota wa mchezo wa masumbwi nchini Mohamed Bawaziri,  na promota wa mpambano wa ubingwa wa Dunia ambao cheka anao kwa sasa Catherini Matili .

MAJI MAREFU AKIWA NA MABINGWA WA MCHEZO WA MASUMBWI NCHINI

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...