BAADHI ya
Mawaziri na askari polisi wametajwa kuwa ni wateja wakubwa wa wanawake wanaouza
miili yao(Machangudoa).
Hayo yameelezwa
na jukwaa la wanaharakati wanawake vijana (YFF), walipokuwa wakiwasilisha
ujumbe wao kwa njia ya sanaa ya ngonjera, katika tamasha la 11 la Mtandao wa
jinsia Tanzania (TGNP) linaloendelea eneo la Mabibo Jijini Dar es Salam.
Wanaharakati
hao wanawake vijana, walisema tatizo lipo kwenye jamii ambayo inawahukumu
machangudoa bila kujiuliza kuwa wateja wa machangudoa hao ni akina nani.
‘’…siku
yakiwanogea twala chipsi na kuku, jamani hebu tuulizane, kwani changudoa mteja
wake nani? Kwa taarifa yako, Mawaziri wamo, wabunge wamo, mapolisi wamo na hii
ni changamoto kwa jamii’’ walisema wanaharakati hao.
Akizungumza
na wanahabari baada ya kutoka jukwaani, kiongozi
wa wanaharakati hao, Aisha Kijavala, amesema wameamua kutoa ujumbe huo kwa
washiriki wa tamasha hilo, ili jamii ijue wateja wa machangudoa hao na kwamba
pindi wao wakiacha kununua ngono, pia wanawake wanaouza miili yao, wataacha
kujiuza.
Tamasha hilo
la 11 ndani ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa shirika lisilokuwa la kiserikali
la Mtandao wa Jinsia Tanzania(TGNP), linatarajia kuisha kesho Septemba 6, mwaka
huu.
Chanzo Kalulunga
No comments:
Post a Comment