Tuesday, April 30, 2013
BABA MZAZI WA CHRIS BROWN, AMEZUNGUMZA KUHUSU MAPENZI YA CHRIS NA RIHANNA
Gazeti la New York Daily News limefanya Exclusive
interview na baba mzazi wa mwimbaji staa Chris Brown na kutoa maoni
yake kuhusu mahusiano ya kimapenzi ya mwanae na Rihanna RiRi. Clinton Brown amesema “sioni maisha marefu kwa Chris Brown kuwa na Rihanna, sijawahi kupendezwa na kurudiana kwao, unajua ni lazima kwenye uhusiano wa kimapenzi uwe na mtu sahihi ambae ni hitaji la kweli na linaloweza kuwa lako kwenye maisha, lakini sio kama hivi” Clinton amesema hapendi kutumia mifano lakini anadhani watu wameona mahusiano ya mastaa kama Whitney Houston, Michael Jackson, Amy Winehouse na wengine” Kuhusu mrembo ambae angependa kuona anaolewa na mwanae, Clinton amemtaja Jordin Sparks kwa kusema “nimempenda Jordin, ni msichana mdogo lakini mwenye upeo mkubwa… ana akili na heshima” |
DOTNATA AFUNGUKA BAADA YA KUGUNDUA KAWEKEWA SUMU KWENYE JUICE
Muigizaji wa
filamu nchini Dotnata Rubagumya anadai kuwekewa sumu kwenye juice na mtu
asiyemfahamu ambayo imemsababishia matatizo makubwa ya kiafya.
Amesema alianza kuhisi kupandwa na pressure ambapo alilazwa
kwenye hospitali ya IMTU na kuambiwa imepanda hadi kufikia 284 huku
wakimweleza huenda ni kwakuwa amenenepa sana.Baadaye alifanyiwa
uchunguzi wa moyo kwenye hospitali ya Lugalo kabla ya kupelekwa TMJ kwa
vipimo zaidi.
Anasema
tatizo hilo lilimsabisha ashindwe kuhema, sauti kukata na mara nyingi
alikuwa akitapika.
“Nimezidiwa usiku wa kuamkia
Jumatano nikakimbizwa tena TMJ ndo sasa ikabidi wanichunguze kwa makini
kwanini nakuwa hivi ndo wakagundua nimelishwa sumu takriban mwezi wa
nane sasa huyo mtu aliyenipa sumu aliipitisha kwa njia ya juice,”
amesema Dotnata ambaye kwa sasa ameokoka.
Akizungumzia
sababu za kuwekewa sumu, Dotnata amesema:
“Kila
mwanadamu ana mawazo jinsi anavyowaza katika akili yake labda
hakupendezewa na mimi niendelea kuishi hivi, labda alifikiria akiniua
mimi yeye hatokufa. Lakini natamka wazi kwamba sitokufa nitaishi ili
niyasimulie mema ya Mungu. Nimejifunza mtu anaweza kuwa rafiki yako
kumbe ndio mbaya wako siwezi kujua ni kwasababu gani, namwachia Mungu.”
Msikilize
zaidi hapa.
NA BONGO CLAN BLOG
NA BONGO CLAN BLOG
Wabunge waliosimamishwa warejea kwa ari Bungeni
Dodoma. Baada ya kutumikia adhabu ya kutohudhuria vikao vitano vya
Bunge, wabunge watano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),
jana waliingia bungeni wakionekana kuwa na ari mpya.
Wabunge waliosimamishwa Aprili 17 ni Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya
Upinzani Bungeni ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu
na Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa.
Wengine ni Highness Kiwia (Ilemela), Ezekiel Wenje (Nyamagana),
Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ (Mbeya Mjini) na Godbless Lema (Arusha Mjini).
Jana
asubuhi Mchungaji Msigwa alikuwa miongoni mwa wabunge waliowahi kuingia
mapema ndani ya Ukumbi wa Bunge na kufuatiwa na Lissu muda mfupi baada
ya kikao kuanza.
Ndani ya Ukumbi wa Bunge, Msigwa
alipata nafasi ya kuuliza swali namba 115 lililokuwa liulizwe na Joyce
Mukya kuhusu Kampuni ya Kamwene Woodworks . Kwa upande wake, Lissu
aliomba mwongozo wa Spika kuhusu kukwama kwa Bajeti ya Wizara ya Maji.
Wabunge wengine haikujulikana sababu za kutofika jana licha ya
kuwa adhabu yao ilikwisha tangu April 25 huku taarifa zikieleza kuwa
Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema alikuwa apelekwe mahakamani kujibu
staka la uchochezi.
Mwananchi
Mitambo ya analojia Mbeya kuzimwa leo saa 6:00 usiku.
Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imesema mitambo ya Analojia mkoani
Mbeya itazimwa rasmi leo saa 6:00 usiku.
Innocent Mungi, alisema Mkoa wa Mbeya.
Akizungumza na waandishi habari jana, Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungi, alisema Mkoa wa Mbeya umekuwa wa mwisho katika hatua za kuzima mitambo hiyo, katika awamu ya kwanza.
Akizungumza na waandishi habari jana, Meneja Mawasiliano wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungi, alisema Mkoa wa Mbeya umekuwa wa mwisho katika hatua za kuzima mitambo hiyo, katika awamu ya kwanza.
Mungi alisema uzimaji wa mitambo ya analojia na kuhamia katika mitambo ya Digitali katika awamu ya kwanza, ulihusisha Mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Tanga, Mwanza, Moshi na Arusha.
Alisema wakazi wa Mbeya walikwishafahamishwa kuhusu kuzimwa kwa mitambo hiyo kwa kufanya maandalizi yaliayohitajika ili kuepuka usumbufu ambao ungejitokeza.
Aliwataka Watanzania kuacha kunung’unika wanapokabiliwa na changamoto mbalimbali na hasa yanayohusu matatizo ya ving’amuzi na badala yake, wachukue za kutafuta ufumbuzi
Alisema baadhi ya Watanzania wamekuwa wakitumia muda mrefu kunung’unika na kushindwa kuchukua hatua za kukabiliana na changamoto zinazowakabili.
Shambulio lafanyika mjini Rome wakati serikali mpya ikiapishwa.
Serikali
mpya nchini Italia imeapishwa na kumaliza hali ya iliyodumu kwa miezi
kadhaa ya wasiwasi wa kisiasa, kufuatia uchaguzi mkuu wa mwezi Februari
mwaka huu, ambao ulishindwa kutoa mshindi wa moja kwa moja.
Hata
hivyo hafla ya kuapishwa kwa viongozi hao ilifunikwa na tukio la
ufyatuaji risasi nje ya ofisi ya waziri mkuu ambapo maafisa wawili wa
polisi walishambuliwa.
Watu
walioshuhudia tukio hilo wamesema walimuona mwanaume mwenye silaha
akifyatua risasi nje ya ofisi ya waziri mkuu katikati ya mji wa Rome,
wakati baraza jipya la mawaziri likiendelea kuapishwa, umbali wa
kilomita moja kutoka hapo, katika ikulu ya rais.
HAWA NDIO WATUMIAJI 11 WA MADAWA YA KULEVYA WENYE AKILI ZAID DUNIANI NA OBAMA YUMO.........!!!
STEVE JOBS
Imeripotiwa
kwamba mwanzilishi wa Apple alitumia madawa kweny muhula wa kwanza kule
Reed College in Portland, Oregon mwaka 1972. Tangu aach shule, Jobs
amekuwa moja ya watu wenye mafanikio zaidi nchini America na dunia nzima
kwa ujumla. Mwaka 1984,medali ya Taifa ya Technology nchini Marekani
kutoka kwa rais wa kipindi hicho Ronald Reagan. Mwaka 2007, Fortune
Magazine walimtaja kama mtu mwenye nguvu zaidi kwenye biashara na kisha
mwaka 2011 gavana wa California Arnold Schwarzeneggerallimuweka kwenye
California Hall of Fame.pia walimtaja kama CEO wa muongo (CEO of the
decade) mwaka 2009 huku Forbeswakimuweka #57 kwenye list ya “World’s
Most Powerful People” mwaka huo huo.
Sir Richard Branson
Huku ile
‘Sir’ikimuweka kwenye list ya watu wanaoheshimiwa zaidi, hiyo sio sababu
ya yeye kuwa kwenye hii list. Kinachomfanywa awekwe ni kwa sababu yeye
anashika namba 236 kwenye watu matajiri zaidi duniani, mwanzilishi wa
Virgin empire, ambayo inashughulika na vitu vingi kuanzia ndege mpaka
maduka ya rekodi tofauti, simu,na ametengeneza utajiri wake from
scratch.Sio tu kwamba a, he gets high with his 21-year-old son.
alishasema mbele ya umati kwamba haoni tatizo kuhusu kutumia
marijuana,na amefanya mchakato kuhalalisha utumiaji wake,na pia amesema
kama ikiruhusiwa, atauza.
DADA WA NDIKUMANA APALILIA NDOA YA KAKA YAKE
Uwoya akiwa na mumewe Ndikumana enzi hizo.
Dada wa mchezaji
wa Timu ya Rayon Sport, Ndikumana Katauti, Fatuma amefunguka kuwa licha
ya migongano ya ndoa ya kaka yake lakini bado wanapendana.
Akizungumza
na gazeti moja la nchini Rwanda, Fatuma alisema kwamba hata ilivyotoka
habari kuwa wifi yake Irene Uwoya amenaswa na Diamond alishtuka sana
kwani yeye bado anaamini ndoa ya kaka yake ina uhai wa asilimia mia
moja.
“Nilishangaa sana kuona
gazeti limeandika kuwa wifi yangu amenaswa na Diamond, mimi naamini
ndoa ya kaka yangu bado ipo hai,” alisema Fatuma.
MH. KOMBANI: WATUMISHI WA UMMA WATAKIWA KUKUZA UCHUMI
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais Manejimenti ya Utumishi wa Umma Celina Kombani amewataka watumishi wa Umma kutimiza wajibu wao ipasavyo ili kukuza uchumi wa nchi.
Waziri Kombani amesema hayo katika ufunguzi wa mkutano wa siku mbili unaohusu majukumu ya watumishi wa Umma katika kutekeleza Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano.
Alisema ubora au udhaifu wa utendaji wa serikali yoyote unahusishwa na ubora wa watumishi wa Umma.
“Uchumi hauwezi kukua bila watumishi wa umma kufanya kazi vizuri, katika kukuza uchumi tunategemea,kukua kwa uchumi pia kunategemea watumishi wa umma,” alisema Waziri Kombani.
Waziri Kombani alisema kwa kipindi cha miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania bara, Tanzania imepiga hatua kubwa katika maendeleo, ingawa inakabiliwa na changamoto mbali mbali.
Pamoja na changamoto hizo, Waziri Kombani amesema Serikali imekuwa ikifanya juhudi mbali mbali ikiwemo, kupitia na kutafakari jinsi ya kufikia malengo ya maendeleo yake kwa haraka zaidi
Alisema changomoto zilizopo katika utumishi huo ni kuwa huduma zinawafikia wananchi kwa polepole, zisizo na ubora mfano kumekuwa na ongezeko la idadi ya wanafunzi wanaondikishwa katika shule ya msingi na sekondari, lakini kuna tatizo la ubora wa elimu.
“Tunapo sema uchumi wa nchi inatakiwa kumwangalia mtu wa ngazi za chini. Hivyo mkutano huu utakuwa unajadili changamoto zilizopo na nini kifanyike,” alisema.
Aidha aliongeza kuwa wakati mwingine wananchi wanalalamikia kuwepo kwa vitendo vya rushwa.
Hata hivyo Waziri Kombani ametoa wito kwa viongozi kutafuta majibu ya changamoto zilizopo, ikiwemo ongozeko la idadi ya watu, matumizi ya rasilimali na matumizi bora ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).
Mkutano huo wa siku mbili, unawashirikisha manaibu makatibu wakuu kutoka wizara mbalimbali, makatibu tawala wa mikoa, wakurugenzi wa Halmashauri, wakuu wa taasisi za elimu ya juu , sekta binafsi na wadau wa maendeleo kutoka ndani na nje ya Tanzania.
Subscribe to:
Posts (Atom)