Rais
Jakaya Kikwete akiangua kicheko wakati walimu (juu), walipokuwa wakipita
kwa maandamano, huku wakiimba ‘Shemeji mshahara bado’ wakati wa sherehe
za Siku ya Wafanyakazi (Mei Mosi) zilizofanyika Uwanja wa Uhuru jijini
Dar es Salaam jana. Walimu walimwita shemeji kwa kuwa mkewe, Salma ni
mwalimu kitaaluma. Picha na Silvan Kiwale.
Dar/mikoani. Rais
Jakaya Kikwete ametoa ahadi mbili za kuwafurahisha wafanyakazi. Kwanza
ametangaza nia ya kuongeza mishahara yao na pili, kupunguza kodi
inayokatwa kwenye mishahara hiyo mambo ambayo ameahidi kutekelezwa
katika Bajeti ya mwaka 2014/2015 inayotarajiwa kuwasilishwa bungeni hivi
karibuni.
Akizungumza
kwenye maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi (Mei Mosi), yaliyofanyika
kitaifa Dar es Salaam jana, Rais Kikwete alisema anatambua kuwa
wafanyakazi wana hamu ya kujua Serikali itasema nini kuhusu masilahi
yao.
Alisema
malalamiko ya wafanyakazi wengi ni kutaka kuona kima cha chini cha
mshahara kinaongezwa huku kodi kwenye mishahara (Paye), ikipungua.
“Mimi na
wenzangu serikalini hatuna upungufu wa dhamira ya kufanya hivyo,
tumethibitisha miaka iliyopita na tutaendelea kuwa hivyo,” alisema. Tafadhari Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz
Huku
akishangiliwa na wafanyakazi waliofurika katika Uwanja wa Uhuru, Rais
Kikwete alisema: “Najua kuwa nyongeza tuliyotoa mwaka jana si kubwa kama
wafanyakazi walivyotaka iwe... hata mimi nisingependa iwe hivyo.”