Monday, July 22, 2013

RATIBA YA LIGI KUU MSIMU UJAO MZUNGUKO WA KWANZA

clip_image001clip_image001[8]

HIZI NDIZO NYUMBA ZITAKAZOSHINDANIWA KATIKA PROMOTION YA AIRTEL YATOSHA

Meneja Mawasiliano wa shirika la nyumba la Taifa Bw, Yahaya Charahani
akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati ambapo waandishi hao walitembelea eneo la kibada wilaya ya Temeke kujionea Nyumba 3 zinazoshindaniwa katika promosheni ya Airtel Yatosha. Nyumba
hizi zimenunuliwa na Airtel toka shirika la nyumba la taifa kwaajili
ya promosheni ya AIRTEL shinda Nyumba.kulia ni Meneja Uhusiano wa
Airtel Bw, Jackson Mmbando
Meneja Uhusiano wa Airtel Bw Jackson Mmbando akiongea na waandishi wa
habari (hawapo pichani) wakati ambapo waandishi hao walitembelea eneo
la kibada wilaya ya Temeke kujionea Nyumba 3 zinazoshindaniwa katika
promosheni ya Airtel Yatosha.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU JULAI 22, 2013 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS

DSC 0047 97a9a

DSC 0048 4d765

MIILI YA ASKARI WA JWTZ WALIOUAWA DARFUR KUAGWA LEO MAKAO MAKUU YA JESHI

 
Askari saba wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), waliouawa katika jimbo la Darfur nchini Sudan, wanatarajiwa kuagwa leo kwenye viwanja vya makao makuu ya jeshi hilo.
Miili ya wanajeshi hao iliwasili nchini juzi kwa ndege maalumu katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J. K Nyerere, Terminal One na kwenda kuhifadhiwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Lugalo jijini Dar es Salaam.
 
Wanajeshi waliouawa ni Sajenti Shaibu Othuman, Koplo Oswald Chaula, Koplo Mohamed Juma, Koplo Mohamed Chikilizo, Rodney Ndunguru, Peter Werema na Fortunatus Msofe.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano, Makao Makuu ya JWTZ, ilieleza kuwa askari hao wataagwa leo na shughuli hiyo itahudhuriwa na familia, makamanda wa jeshi na viongozi wa Serikali.

LOWASSA, DK. SLAA, MEMBE WAWEKWA NJIA PANDA KUWANIA URAIS.....!!!

*Rasimu kutumika kuwaondolea sifa ya kugombea urais
*Yumo pia Membe, Magufuli, Sitta, Zitto na Wassira


Freeman Mbowe

Dk. Wilbrod Slaa
MKAKATI wa kuwaengua vigogo wanaotajwa kung’ang’ania kugombea nafasi ya Urais katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 sasa umebainika, MTANZANIA Jumapili linaripoti.

 Kwa mujibu wa uchunguzi wa kina uliofanywa na gazeti hili,    mkakati huo ambao umelenga kuwang’oa viongozi hao,  unadaiwa kutekelezwa na baadhi ya wanasiasa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Rasimu ya Katiba Mpya, iliyotolewa hivi karibuni na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.



Dk. Emmanuel Nchimbi


Steven Wassira
Imeelezwa kuwa kupitia Rasimu hiyo ya Katiba Mpya, kuna vipengele vilivyopenyezwa kwa nia ya kuwabana watu fulani fulani ndani na nje ya CCM ambao wanatajwa kuusaka ukuu wa dola mwaka 2015 na chama hicho hakitaki kuona wanakuwa kikwazo dhidi yake.

Mtoa habari wetu ndani ya CCM alilidokeza gazeti hili kuwa vipengele hivyo ambavyo vimewekwa kama mtego, ni vile vinavyotaja sifa za mgombea Urais na mgombea Ubunge.


January Makamba


Bernard Membe
Kwa mujibu wa taarifa zilizotufikia, kutokana na hilo, baadhi ya wanasiasa ndani ya CCM kwa makusudi wameamua kuufanya mjadala kuhusu serikali tatu kuwa mkali, ili kuzuia mjadala mpana katika masuala mengine.

Kipengele ambacho kama kikiachwa bila kufanyiwa marekebisho kinaweza kuwabana wanasiasa wengi ndani na nje ya CCM wanaotajwa kuwania Urais 2015 ni pamoja na kile cha Sura ya Saba, ambacho kinazungumzia Serikali ya Jamhuri ya Muungano kuhusu Serikali, Rais na Makamu wa Rais, katika sehemu ya kwanza C kwenye kipengele cha 75 (E) kinachozungumzia sifa za Rais kimeeleza kuwa mtu atakuwa na sifa ya kuchaguliwa kushika nafasi ya madaraka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano ikiwa: anazo sifa za kumwezesha kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa Katiba hiyo.

SAMAKI WALIOVULIWA KWA MABOMU NA SUMU WATAPAKAA KWENYE MASOKO JIJINI DAR ES SALAAM


Wakazi wa jiji la Dar es Salaam, wameambiwa wachukue tahadhari na umakini wakati wa kununua samaki nyakati za jioni, kutokana na madai kuwa baadhi ya wachuuzi huvua kwa kutumia mabomu.

Tahadhari hiyo imekuja baada ya kufanya uchunguzi wa muda mrefu, ambapo imegundua samaki hao wanauzwa nyakati hizo kukwepa kugundulika.
Imefahamika licha ya Serikali kuwa na kampeni ya kusaka watu wanaojihusisha na uvuvi huo, bado hali imekuwa mbaya katika maeneo ya pwani ya bahari ya Hindi.


Maeneo yanayotajwa kukithiri kwa uvuvi wa mabomu ni Pwani ya Bagamoyo, Kawe katika Manispaa ya Kinondoni na Buyuni eneo la Kigamboni, Manispaa ya Temeke.

Baadhi ya wavuvi waliofanikiwa kuzungumza na gazeti hili kwa masharti ya kutotajwa majina yao kwa usalama, walisema watu wanaojihusisha na uvuvi haramu wanatumia mbinu nyingi za kuingiza samaki sokoni.
Walisema watu wengi kutokana na kuanza kuwabaini samaki wa aina hiyo, wavuvi wanawauza kwenye maeneo ya mikusanyiko ya watu nyakati za jioni bila ya kugundulika kwa urahisi.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...