Sunday, April 14, 2013
TAMKO LA CHADEMA KUHUSU NJAMA ZA KUKICHAFUA ZINAZOFANYWA NA GENGE LA VIONGOZI WAKUU WA CCM NA VYOMBO VYA DOLA
Ndugu waandishi wa habari;
LEO
tumewaita hapa ili kuwaomba mtufikishie ujumbe kwa Watanzania, kwamba
nikiwa mwanasheria na mtu ambaye nimepata ujuzi wa kazi za ushushu,
nimefanya uchunguzi matukio haya ya utekaji na utesaji na kugundua mambo
mengi mno.
Uchunguzi huu
nimeufanya kabla na baada ya kukamatwa kwa Mkurugenzi wetu wa Ulinzi na
Usalama, Willifred Muganyizi Lwakatare, ambaye hivi sasa anashitakiwa
mahakamani kwa tuhuma za kupanga ugaidi.
Nimefanya hivyo
kwa kuangalia maslahi mapana ya taifa langu na chama changu. Katika
uchunguzi wangu huo, nimegundua mambo mengi ikiwamo kuwapo kwa genge la
watu ndani ya serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM), wanaopanga mipango
hii ya kishetani na kisha kuwasingizia watu wengine.
Angalieni mfano huu: Unaoitwa na polisi
na Mwigulu Nchemba, “mkanda wa Lwakatare” unadaiwa uliwasilishwa jeshi
la polisi Desemba mwaka jana. Lakini jeshi hilo halikumkamata yoyote
wala kumhoji, hadi pale Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom
Kibanda, alipovamiwa na kuumizwa.
Aidha, Nchemba amedai kumiliki video
ile Desemba mwaka jana, lakini rekodi hiyo iliwekwa kwenye mitandao ya
kijamii (YouTube na Jamii Forum) baada ya kutekwa kwa Kibanda. Hapa mtu
makini anaweza kujiuliza, hiki kimelenga nini?
JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA Taarifa kwa Vyombo vya Habari
14
Aprili, 2013
Jeshi la
Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linasikitika kutangaza kifo cha
Meja Jenerali Rashid Mnalihinga Makame (mstaafu) ambaye amefariki dunia
tarehe 14 Aprili, 2013 saa kumi na mbili na nusu asubuhi, katika
Hosptali ya TMJ.
Pamoja
na nyadhifa mbalimbali alizowahi kushika Jeshini na Serikalini, Meja
Jenerali Rashid Mnalihinga Makame (mstaafu) alikuwa Mkuu wa JKT wa
tano. Kama mnavyofahamu umuhimu wa JKT, yeye ni miongoni mwa Makamanda
walioleta tija kubwa katika kuwalea Vijana wa Kitanzania na kuwajengea
nidhamu na uzalendo.
Mpango
wa Mazishi unafanywa, mtajulishwa baadae juu ya wapi na lini atazikwa
Meja Jenerali Rashidi Mnalihinga Makame (Mstaafu). Msiba upo nyumbani
kwake Mikocheni, karibu na nyumbani kwa Hayati Mwl J.K Nyerere.
MUNGU AILAZE MAHALI PEMA PEPONI
ROHO YA MAREHEMU
Meja
Jenerali Rashidi Mnalihinga Makame (MSTAAFU) AMINA.
Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao
Makuu ya Jeshi, Upanga
SLP
9203, Simu: 0764-742161
Email:ulinzimagazine@yahoo.co.uk
Chadema yatishia kujitoa mchakato wa Katiba Mpya
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema kitajitoa
katika mchakato wa Katiba Mpya endapo mambo muhimu mawili hayatapatiwa
ufumbuzi hadi kufikia Aprili 30, mwaka huu.
Wakati Chadema wakisema hayo, Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata), limesema uchaguzi wa wajumbe wa Mabaraza ya Katiba uliomalizika siku tatu zilizopita katika maeneo mbalimbali nchini haukuwa huru na ni batili, huku likipendekeza urudiwe katika maeneo yote yaliyokumbwa na kasoro.
Katika hoja zake, Chadema kimesema kinataka kufutwa kwa uteuzi/uchaguzi wa wajumbe wa Mabaraza ya Wilaya ya Katiba uliofanywa na Kamati za Maendeleo za Kata na badala yake wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya wachaguliwe moja kwa moja na wananchi wa Kata husika bila kuchujwa na Kamati za Maendeleo za Kata (WDC).
Wakati Chadema wakisema hayo, Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata), limesema uchaguzi wa wajumbe wa Mabaraza ya Katiba uliomalizika siku tatu zilizopita katika maeneo mbalimbali nchini haukuwa huru na ni batili, huku likipendekeza urudiwe katika maeneo yote yaliyokumbwa na kasoro.
Katika hoja zake, Chadema kimesema kinataka kufutwa kwa uteuzi/uchaguzi wa wajumbe wa Mabaraza ya Wilaya ya Katiba uliofanywa na Kamati za Maendeleo za Kata na badala yake wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya wachaguliwe moja kwa moja na wananchi wa Kata husika bila kuchujwa na Kamati za Maendeleo za Kata (WDC).
Msimamo huo ulitolewa na Msemaji Mkuu wa
Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe wakati akisoma hotuba yake ya
makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2013/14 huku akiitaka
Serikali kuwasilisha muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Katiba ili
maeneo kadhaa yafanyiwe marekebisho.
MWANAMKE ANUSURIKA KUUAWA NA PADRI AMBAYE NI MPENZI WAKE HUKO KIBAHA......!!
( picha na maktaba)
Bi Celestina
Ananius(35) amenusurika Kuuawa na Padri wa kanisa katoliki parokia ya Hombolo iliyoko Dodoma kwa jina
la Celestine John Nyaumbana ambaye kwa Sasa anaishi kwenye Makazi ya Katoliki Mbezi kwa
ajili ya Masomo.
Dada huyo
anasema amekuwa katika mapenzi na padri huyo tangia akiwa Fratel, akawa
Shemasi na sasa ni padri na suala hilo ni siri yao na wazazi wa pande
mbili hadi wamezaa mtoto anaitwa Agnes (3).
Bi Celestina ambaye anaishi Dodoma alikuja Dar kumfuata Mpenzi wake huyo ili ajue hatima ya huyo mtoto wao....
Sasa wakati wapo Dar padri huyo alimuomba mpenzi wake huyo watoke kidogo kwenda kutembea maeneo ya Kiluvya...
Walipofika huko wakati wapo katikati ya
pori padri huyo alishuka kwenye gali na kumshambulia dada huyo kwa
madhumuni ya kumuua na kupoteza ushaidi ila hakufanikiwa kumuua .....
Taarifa za Polisi Mkoa wa Pwani zinaonyesha kuwa Mwanamke huyo aliokolewa na Wasamalia wema na kukimbizwa Hospitali ya Tumbi Kibaha kwa matibabu!!!
source: Police Kibaha na Wapo radio kipindi cha Patapata
MAJID MJENGWA NAYE AKAMATWA NA POLISI AKIHUSISHWA NA SAKATA LA KIBANDA.....!!
Majid Mjengwa.
MWANDISHI wa safu katika magazeti
mbalimbali nchini, Majid Mjengwa amekamatwa na polisi kwa tuhuma za
kuhusika na tukio la kushambuliwa kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri
Tanzania (TEF), Absalom Kibanda.
Habari zilizoufikia mtandao huu jana mchana na baadaye
kuthibitishwa na polisi zinasema Mjengwa alikamatwa muda wa asubuhi na
kwamba alikuwa akihojiwa na makachero wa jeshi hilo hadi alasiri
kuhusu tukio la kuteswa kwa Kibanda.
Msemaji Mkuu wa Polisi Advera Senso alisema kwamba:
“Ni kweli kwamba tunaye, tunaendelea kumhoji, tunachoomba ni
kwamba mtupe nafasi ili tufanye kazi yetu na kukiwa na jambo lolote
tutawajulisha.”
Subscribe to:
Posts (Atom)