Wednesday, March 19, 2014

CCM YAZINDUA KAMPENI KWA KISHINDO CHALINZE

 Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimnadi mgombea wa Ubunge katika uchaguzi mdogo jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete, katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM uliofanyika leo kwenye Uwanja wa  Miembesaba, Chalinze mkoa wa Pwani. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz 
Mgombvea ubunge katika uchaguzi mdogo jimbo la Chalinze, kwa tiketi ya CCM, Ridhiwani Kikwete akiomba kura katika mkutano wa uzinduzi wa kampeni za CCM za uchaguzi huo leo kwenye Uwanja wa Miembe saba, Chalienze.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz 

MAGAZETI YA LEO JUMATANO MARCH 19, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


..



RAIS KIKWETE KUHUTUBIA BUNGE IJUMAA WIKI HII

D92A0027_3d92f.jpg
Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuhutubia Bunge Maalum Machi 21 mwaka huu mjini DodomaKauli hiyo imetolewa leo na Katibu wa bunge hilo, Yahya Khamis Hamad wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa waandishi wa habari wa ofisi za Bunge mjini Dodoma.
"Kwa mujibu wa kanuni ya 75 (1), Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atalihutubia Bunge Maalum siku ya Ijumaa Machi 21 ,mwaka 2014 saa 10:jioni, ambapo wageni waalikwa wote watatakiwa kuwa wameingia na kuketi katika maeneo watakayoelekezwa saa 9:00 alasiri," alisema Katibu huyo.
Aidha Katibu huyo alisema ratiba ya shughuli hiyo itaanza na kikao cha Bunge saa 9:10 na baadae kikao hicho kitaanza saa 9:20 kwa ajili ya kumpokea Rais.
Aliongeza kuwa mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Bunge, Rais Kikwete atapokewa na Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu, Naibu Katibu wa Bunge Maalum, ambapo baadae ataelekea katika jukwaa maalum kwa ajili ya kupokea salamu za heshima na kukagua Gwaride Maalum ambalo limeandaliwa na jeshi la polisi.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz 

MCHINA AFUNGWA JELA MIAKA 20 KWA KUKUTWA NA MENO YA TEMBO

Suleiman-Kova-March19-2014_a498c.png
Kamanda Kanda Maalum, Seleman Kova akiwa ameshika meno ya tembo.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemhukumu raia wa China, Yu Bo (45), kulipa faini ya Shilingi bilioni tisa au kwenda jela miaka 20 baada ya kukiri kukutwa na nyara za serikali.
Yu, alikamatwa akiwa na kilo 303 za nyara hizo ikiwamo ngozi za vinyonga wawili vyote vikiwa na thamani ya Sh. milioni 975 mali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mkazi, Devota Kisoka, baada ya upande wa Jamhuri kumsomea mshtakiwa mashitaka na kukiri.
Alisema baada ya mshtakiwa kukiri makosa yake, mahakama imemtia hatiani na kumhukumu kulipa faini ya Shilingi bilioni tisa na akishindwa aende jela miaka 20.

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz 

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...