Tuesday, August 20, 2013
AJARI KATIKA MSAFARA WA MBIO ZA MWENGE DODOMA
KIM AITA 24 STARS KUIVAA GAMBIA
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen ameita kambini wachezaji 24
kujiandaa kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Gambia
itakayochezwa Septemba 7 mwaka huu nchini humo.
Wachezaji hao wanatakiwa kuripoti kambini Agosti 29 mwaka huu kabla ya saa 1 kamili usiku. Kambi ya Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itakuwa kwenye hoteli ya Accommondia jijini Dar es Salaam.
Wachezaji hao wanatakiwa kuripoti kambini Agosti 29 mwaka huu kabla ya saa 1 kamili usiku. Kambi ya Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itakuwa kwenye hoteli ya Accommondia jijini Dar es Salaam.
Makipa walioitwa katika timu hiyo Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ali (Azam), Ally Mustafa (Yanga) na Aishi Manula (Azam). Mabeki ni Aggrey Morris (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Shomari Kapombe (Simba), Nadir Haroub (Yanga), Erasto Nyoni (Azam), Vincent Barnabas (Mtibwa Sugar) na David Luhende (Yanga).
Viungo Khamis Mcha (Azam), Salum Abubakar (Azam), Said Dilunga (Ruvu Shooting), Frank Domayo (Yanga), Athuman Idd (Yanga), Haruna Chanongo (Simba), Amir Kiemba (Simba), Mrisho Ngasa (Yanga), Simon Msuva (Yanga), John Boko (Azam), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo) na Juma Liuzio (Mtibwa Sugar).
MWALIMU WA MIAKA 30 AMWEKA KUNYMBA MWANAFUNZI WA MIAKA 14....!!!

MWANAFUNZI wa darasa la saba katika Shule ya Msingi ya Sokoine, Manispaa ya Dodoma (jina linahifadhiwa), anadaiwa kuwekwa kinyumba na mwalimu wake David Macha (30).
Mwanafunzi huyo wa miaka 14 ni kati ya watoto wanaofadhiliwa na shirika lisilo la kiserikali la Compassion International Tanzania kituo cha Tz 807 FPCT kilichoko Chamwino.
Hata hivyo, katika hali ya kushangaza Jeshi la Polisi mkoani hapa, limelalamikiwa na wazazi wa mtoto huyo kwa kitendo cha kumlinda mtuhumiwa licha ya kupewa taarifa za uhalifu huo kwa zaidi ya miezi mitano sasa, limeshindwa kumchukulia hatua.
Uchunguzi wa Tanzania Daima ambao umethibitishwa na wazazi wa mwanafunzi huyo, umebaini kuwa mwalimu Macha amekuwa akifanya mapenzi na mwanafunzi huyo kwa zaidi ya miezi mitano sasa.
Wazazi wa mwanafunzi huyo wanathibitisha kuwa kwa zaidi ya miezi mitano, mtoto wao alikuwa na tabia ya kutoroka nyumbani nyakati za usiku na kulala nje, jambo ambalo lilianza kuwatia mashaka na kuanza kufuatilia nyendo zake.
Walidai kuwa wakati mwingine alikuwa akirudi nyumbani asubuhi kwa ajili ya kujiandaa kwenda shule na anapoulizwa alikolala, alisema alikuwa katika mkesha.
Akisimulia mkasa huo, mjomba wa mwanafunzi huyo, Silas Mjengi, alisema binti yao anaishi na mama yake pekee katika eneo la Area ‘A’ mjini hapa baada ya mzazi huyo kutengana na mumewe.
"MWAKYEMBE ALINDWE" BARAZA LA VIONGOZI WA DINI

Mwenyekiti wa baraza la viongozi wa dini la kupambana na dawa za kulevya nchini Shekhe wa mkoa wa Dar es Salaam Alhad Mussa Salum
BARAZA la Viongozi wa Dini la Kupambana na Dawa za Kulevya nchini, limetaka Jeshi la Polisi kumpa ulinzi Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe, kutokana wa ujasiri alioonesha kupambana na dawa za kulevya.
Kutokana na ujasiri huo, Baraza hilo ambalo Mwenyekiti wake ni Shekhe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, limempongeza Dk Mwakyembe na kusisitiza umuhimu wa ulinzi huo kwake, kwa kuwa vita aliyoanza, inaweza kuhatarisha usalama wake.
Shekhe Salum alisema hayo jana alipozungumza na vyombo vya habari Dar es Salaam, akiongeza kuwa kitendo alichofanya waziri huyo kimeonesha uzalendo, ujasiri na upendo alionao kwa Taifa, alilosema linalochungulia kaburi kutokana na dawa hizo.
Maombi maalumu
Kutokana na ujasiri huo na hatari inayomkabili Dk Mwakyembe, pamoja na kutaka ulinzi wa Polisi, Shekhe Salum pia aliomba viongozi wa dini wa imani zote, kumwombea kwa uthubutu huo. Alisema watampa ushirikiano kwa kuunga mkono juhudi anazoonesha ambazo kwa kiasi kikubwa anaamini zitarejesha heshima ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNIA).
“Kwa dhati kabisa Baraza linataka mawaziri na viongozi nchini kuiga mfano wake, ili kuliondoa Taifa letu katika sifa mbaya ya dawa za kulevya,” alisema Shekhe Salum.
Kwa mujibu wa kiongozi huyo, viongozi wana uwezo mkubwa wa kujitolea kupambana na dawa hizo, isipokuwa hakuna aliye tayari kuonesha uthubutu wake, suala alilosema kwa kiasi kikubwa limechangia mapambano dhidi ya dawa hizo kutofanikiwa.
MTANDAO WA KAGAME WAZIDI KUMCHOKOZA KIKWETE.... WADAI MAMA SALMA KIKWETE NI MNYARWANDA...!!!

Mtandao wa News of Rwanda umeendelea kutuchokonoa watanzania ili kuupima msimamo wetu.....
Baada ya kukurupuka na madai kwamba Rais Kikwete si mtanzania halisi na kwamba ni mtu mwenye asili ya Burundi, mtandao huo umekuja na kioja kipya....
Taarifa iliyotolewa jana tarehe 19/08/2013 na mtandao huo inadai kwamba mke wa Rais Kikwete aitwaye Mama Salma Kikiwete ni mnyarwanda wa kabila la wahutu ( mhutu )..
Katika maelezo yake, mtandao huo umeenda mbali na kudai kuwa Mama Salma Kikwete ni binadamu wa rais wa zamani wa Rwanda, Juvenal Habyarimana na ndo maana rais Kikwete alitoa ushauri wa mazungumzo ya amani kati ya Kagame na waasi....
VIGOGO WAJUMUISHWA KESI YA LEMA....!!!

Mkuu wa Chuo cha Uhasibu cha Arusha, John Nanyaro na Mkuu wa
Polisi wa Wilaya ya Arusha, Gillis Mroto, leo wanaanza kutoa ushahidi
katika kesi ya tuhuma za uchochezi inayomkabili Mbunge wa Arusha Mjini,
Godbless Lema.
Mashahidi wengine katika kesi hiyo ni, Mkaguzi wa Polisi Bernard Nyambanyana na mwenzake aliyetajwa kwa jina moja la Jane.
Hali kadhalika PC Godfrey na Joachim Mahanyu .
Wakili wa Serikali, Elinenya Njiro, alitaja mashahidi wengine watakaotoa
ushahidi wao mahakamani kuwa Faraji Mnepe, Benjamin Simkanga na Naibu
Hamidu, wote kutoka Chuo cha Uhasibu.
SHOMARY KAPOMBE KUJIUNGA NA AS CANNES YA UFARANSA

Hatimaye beki wa kimataifa wa klabu ya Simba na timu ya taifa ya Tanzania Shomary Kapombe amefuzu majaribio aliyokuwa akifanya barani ulaya kwa kufanikiwa kujiunga na klabu ya AS Cannes ya Ufaransa.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka mwandishi wa BBC - Abdul Mohamed ni kwamba Shomary Kapombe amefuzu majaribio hayo na sasa zimebakia taratibu tu za uhamisho ili ajiunge rasmi na timu hiyo ya AS Cannes inayoshiriki kwenye ligi daraja la nne nchini Ufaransa.
Kapombe aliondoka nchini takribani mwezi mmoja uliopita na kwenda barani ulaya kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa.
Mtandao huu upo katika kujaribu kufanya mawasiliano na uongozi wa Simba ili kupata taarifa rasmi juu ya usajili huu wa Shomary Kapombe.Credits: Shaffih Dauda Blog
Kwa mujibu wa taarifa kutoka mwandishi wa BBC - Abdul Mohamed ni kwamba Shomary Kapombe amefuzu majaribio hayo na sasa zimebakia taratibu tu za uhamisho ili ajiunge rasmi na timu hiyo ya AS Cannes inayoshiriki kwenye ligi daraja la nne nchini Ufaransa.
Kapombe aliondoka nchini takribani mwezi mmoja uliopita na kwenda barani ulaya kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa.
Mtandao huu upo katika kujaribu kufanya mawasiliano na uongozi wa Simba ili kupata taarifa rasmi juu ya usajili huu wa Shomary Kapombe.Credits: Shaffih Dauda Blog
KESI YA MWANARIADHA OSCAR PISTORIUS ALIYEMUUA MPENZI WAKE KWA KUMPIGA RISASI ITAANZA MACHI MWAKANI....!!!

Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius amefika mahakamani ambapo ameshtakiwa kwa mauaji ya mpenzi wake.
Oscar Pistorius alizingirwa na umati mkubwa wa waandishi wa habari alipofika mahakamani mji wa Pretoria. Akiandamana na jamaa wake mwanariadha huyo alifanya maombi maalum. Punde baada ya kusomewa makosa ya kumuua Mwanamitindo Reeva Steenkamp, Oscar alionekana kupatwa na huzuni kubwa.
Subscribe to:
Posts (Atom)