Saturday, May 14, 2016

HII NDIO YANGAAA.... WAKABIDHIWA RASMI KOMBE LA UBINGWA WA VPL

Waziri wa Kilimo na Mifugo Mh. Mwigulu Nchemba (kushoto) ambaye alikuwa mgeni rasmi wa mchezo huo akikabidhi kombe hilo kwa nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ baada ya kumalizika kwa mchezo kati ya Ndanda FC Yanga dhidi ya Yanga uliomalizika kwa timu hizo kutoka sare ya kufungana magoli 2-2.
Kikosi cha Yanga wakishangilia baada ya kukabidhiwa kombe lao.
Donald Ngoma (kushoto) na Simon Msuva wakipongezana wakati wa mchezo wa leo.
Yanga imekabidhiwa taji lao la ubingwa wa VPL msimu wa 2015-16 baada ya kufanikiwa kulitetea taji hilo ambalo walilitwaa msimu uliopita. Yanga imepewa kombe hilo ikiwa na pointi 74 huku ikiwa na mchezo mmoja mkononi baada ya kuifunga Ndanda FC kwenye uwanja wa taifa.

Ndanda walianza kupata goli kwa mkwaju wa penati Omary Mponda lakini bao hilo lilisawazishwa na Simon Msuva dakika chache baadaye. Donald Ngoma akaifungia Yanga bao la pili na kuiweka mbele klabu yake lakini Salum Minely akachomoa bao hilo na kuilazimisha Yanga kwenda sare kwenye uwanja wa taifa ambao Ndanda ndiyo walikuwa wenyeji katika mchezo huo. 
Waziri wa Kilimo na Mifugo Mh. Mwigulu Nchemba ambaye alikuwa mgeni rasmi wa mchezo huo alilikabidhi kombe hilo kwa nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ baada ya kumalizika kwa mchezo kati ya Ndanda FC Yanga dhidi ya Yanga uliomalizika kwa timu hizo kutoka sare ya kufungana magoli 2-2. 

Ubingwa huo unawafanya Azam FC kulikosa taji hilo ndani ya misimu miwili mfululizon wakati Simba wao wameendelea kulikosa taji hilo ndani ya misimu minne mfululizo.

KAGAME AKANA KUWASAIDIA WAASI WA BURUNDI


Rais wa Rwanda Paul Kagame

Rais wa Rwanda Paul Kagame amekana madai yaliotolewa na Umoja wa Mataifa kwamba taifa lake linaendelea kuwasaidia waasi katika nchi jirani ya Burundi.

Kagame amesema kuwa tatizo la Burundi linatoka ndani ya nchi hiyo, na sio nje. Burundi imekabiliwa na mgogoro mbaya wa kisiasa tangu rais Pierre Nkurunziza kuamua kupigania muhula mwengine mwaka uliopita.

Ni mwaka mmoja kamili tangu rais Nkurunziza kuepekua jaribio la mapinduzi. Rwanda ilikana madai kama hayo kuhusu kuwaunga mkono waasi katika ripoti ya awali ya Umoja wa Mataifa mnamo mwezi Februari.

Pia Kagame amekosoa wachapishaji wa ripoti hiyo ambayo inatarajiwa kuwasilishwa katika baraza la usalama la Umoja wa Mataifa baadaye,ikisema mda wake ungetumika vyema kuangazia matatizo yanayokumba mataifa badala ya kuyazidisha. 

Ripoti hiyo iliopatikana na chombo cha habari cha Reuters imeishtumu Rwanda kwa kutoa mafunzo pamoja na usaidizi wa kifedha kipindi chote cha mwaka 2016 kwa waasi wanaolenga kumuondoa madarakani rais Pierre Nkurunziza.

UN "UHUSIANO WA IS NA BOKO HARAM NI TISHIO"


Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeelezea wasiwasi wake kuhusu kasi ya kuimarika kwa ushirikiano kati ya kundi la wapiganaji la Boko Haram nchini Nigeria na lile la Islamic State, wakati Nigeria inaandaa kongamano la kupambana na kundi hilo la kigaidi.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, baraza hilo la wanachama 15 limesema kuwa Boko Haram linaendelea kuwa tishio kwa amani na usalama wa mataifa ya Afrika Magharibi na Afrika ya kati.

Boko Haram lilitangaza utiifu wake kwa Islamic State mwaka jana, na inaripoitiwa kuwa liliwatuma wapiganaji wake kuungana na Islamic State nchini Libya. 

Baraza hilo pia limekaribisha kongamano lililoandaliwa na rais wa Nigeria Mohamadu Buhari siku ya Jumamosi, kuangazia upya jitihada za kupambana na wapiganaji hao. Kongamano hilo litahudhuriwa na viongozi wa kikanda pamoja na rais wa ufaransa Francois Hollande.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...