Kagame amesema kuwa tatizo la Burundi
linatoka ndani ya nchi hiyo, na sio nje. Burundi imekabiliwa na mgogoro mbaya
wa kisiasa tangu rais Pierre Nkurunziza kuamua kupigania muhula mwengine mwaka
uliopita.
Ni mwaka mmoja kamili tangu rais Nkurunziza
kuepekua jaribio la mapinduzi. Rwanda ilikana madai kama hayo kuhusu kuwaunga
mkono waasi katika ripoti ya awali ya Umoja wa Mataifa mnamo mwezi Februari.
Pia Kagame amekosoa wachapishaji wa ripoti
hiyo ambayo inatarajiwa kuwasilishwa katika baraza la usalama la Umoja wa
Mataifa baadaye,ikisema mda wake ungetumika vyema kuangazia matatizo
yanayokumba mataifa badala ya kuyazidisha.
Ripoti hiyo iliopatikana na chombo cha habari
cha Reuters imeishtumu Rwanda kwa kutoa mafunzo pamoja na usaidizi wa kifedha
kipindi chote cha mwaka 2016 kwa waasi wanaolenga kumuondoa madarakani rais
Pierre Nkurunziza.
No comments:
Post a Comment