Katika taarifa kwa vyombo vya habari, baraza
hilo la wanachama 15 limesema kuwa Boko Haram linaendelea kuwa tishio kwa amani
na usalama wa mataifa ya Afrika Magharibi na Afrika ya kati.
Boko Haram lilitangaza utiifu wake kwa
Islamic State mwaka jana, na inaripoitiwa kuwa liliwatuma wapiganaji wake
kuungana na Islamic State nchini Libya.
Baraza hilo pia limekaribisha kongamano
lililoandaliwa na rais wa Nigeria Mohamadu Buhari siku ya Jumamosi, kuangazia
upya jitihada za kupambana na wapiganaji hao. Kongamano hilo litahudhuriwa na
viongozi wa kikanda pamoja na rais wa ufaransa Francois Hollande.
No comments:
Post a Comment