Snura amewaomba radhi watanzania kwa video ya wimbo wake ‘Chura’ inayowadhalilisha wanawake na iliyo kinyume na maadili. Muimbaji huyo amekutana na waandishi wa habari Alhamis hii kwenye ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dar es Salaam.
Jana
video na wimbo huo vilifungiwa na wizara ya habari, utamaduni, sanaa na
michezo kwa madai kuwa inakiuka maadili ya Kitanzania. Pia alizuiwa
kufanya maenesho ya hadhara kwakuwa hajajisajili kwenye baraza la sanaa
la taifa, BASATA.
Kwenye
mkutano huo na waandishi wa habari, Snura amedai kuwa tayari
amekamilisha mchakato wa usajili na BASATA imempa kibali. Pia amedai
kuwa amewasilisha video mpya ya wimbo huo kwa bodi ya filamu ya Tanzania
ambayo itaikagua. Tangaza
biashara yako hapa. Pia like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow
instagram @jambotz.
No comments:
Post a Comment