Mwanasiasa mashuhuri nchini Jamhuri
ya Demokrasi ya Congo Moise Katumbi amethibitisha kuwa atagombea urais
kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba.
Mfanyabiashara
huyo na gavana wa zamani wa jimbo la Katanga alitoa
tangazo hilo kupitia kwa mitandao ya kijamii. Muungano wa vyama kadha
vya upinzani uliamua kumuidhinisha Bw Katumbi kuwa mgombea mwezi Machi.
Bw Katumbi, akitangaza kuwania kwake, amepuuzilia mbali madai kwamba
alipokuwa waziri wa hati alitumia mamluki kutoka nje akisema habari hizo
ni za uongo. Kwa mujibu wa
katiba ya nchi hiyo Rais Joseph Kabila anatakiwa kuondoka madarakani
mwaka huu lakini wapinzani wake wana hofu kuwa huenda ana mipango ya
kusalia madarakani.
No comments:
Post a Comment