Serikali imesitisha wimbo na video ya ‘Chura’ wa msanii,
Snura Mushi ‘Snura Majanga’, kuchezwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari hadi
itakapofanyiwa marekebisho. Wimbo na video hiyo umetokana na maudhui ya
utengenezwaji wake ambayo hayaendani na maadili ya Mtanzania. Tangaza biashara
yako hapa. Pia like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow
instagram @jambotz.
Pia Serikali imesitisha maonyesho yote ya
hadhara ya msanii huyo, mpaka atakapokamilisha taratibu za usajili wa kazi zake
za sanaa katika Baraza la Sanaa la Taifa (Basata). Licha ya hivyo, Serikali
imewataka wasanii wajiulize kabla ya kubuni kazi zao za sanaa kwa kufikiria
wazazi, ndugu, jamaa na marafiki zao namna watakavyozipokea.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano
serikalini, Zawadi Msalla, aliwaambia waandishi wa habari kwamba wasanii
wanapotunga nyimbo zao wavae nafasi za wanaowadhalilisha na waelewe kwamba
sanaa si uwanja wa kudhalilisha watu. Tangaza biashara yako hapa. Pia like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow
instagram @jambotz.
“Serikali imechukizwa na kazi hiyo ya Snura kwa
kuwa si tu inadhalilisha tasnia ya muziki, bali inadhalilisha utu wa mwanamke
kiasi kwamba jamii inaanza kuhoji hadhi ya msanii, weledi na taaluma ya sanaa
kwa ujumla,” alieleza Msalla.
Msalla aliongeza kwa kuwataka wananchi
kutojiingiza katika makosa ya sheria ya mtandao, kwa kusambaza wimbo huo kwa
njia yoyote ya kimtandao. Pia alivitaka vyombo vya habari viwe vya kwanza
kuchuja maudhui ya kazi za sanaa, kabla ya kuwa mawakala wa uharibifu wa jamii
kupitia kucheza kazi chafu za sanaa.
Hata hivyo, inadaiwa baada ya Snura kuitwa na
Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo kwa ajili ya utetezi wake
alishindwa kujieleza alipotakiwa kueleza anajisikiaje kumdhalilisha mwanamke
wakati yeye ni mwanamke. Inadaiwa Snura alikosa la kujibu zaidi ya kuomba
msamaha kwa Serikali imsamehe kwa alichokifanya.
Snura alipotakiwa na Mtanzania kuelezea
alivyopokea kifungo hicho, alidai kwamba atazungumza na waandishi wa habari leo
katika mkutano wake. “Leo (jana) sizungumzi chochote na waandishi nitazungumza
kesho (leo) katika mkutano wangu pale Idara ya Habari Maelezo nitatoa yangu,”
alieleza Snura.
Kabla wimbo huo haujatoka, Snura alikuwa akipiga
picha za vipande vikimuonyesha akiwa maeneo mbalimbali akitikisa umbo lake
akimuwakilisha chura. Baadhi ya vipande hivyo alivionyesha kama chura akiwa
anafua, anapika, anaumwa ametundikiwa dripu na nyinginezo jambo ambalo lilizua
maswali mengi ya kuhusu maadili ya Mtanzania kwa mashabiki wake na wadau wa
muziki kwa ujumla.
Wimbo wa video hiyo inakuwa ya pili kwa msanii
huyo kufungiwa kutokana na maadili mabovu, ambapo awali video ya Snura
‘Majanga’ ulifungiwa na kutolewa katika kinyang’anyiro cha vipengele vya
kugombea tuzo za muziki za Kili huku mwenyewe akilalamika kutotendewa haki.
Pamoja na wimbo huo, wimbo mwingine uliotolewa
katika mchakato huo na kufungiwa pamoja na ‘Majanga’ ni video ya wimbo wa
‘Uzuri wako’ ya msanii, Juma Jux. Nyimbo nyingine zilizowahi kufungiwa kutokana
na kukiuka maadili ya Mtanzania ni ‘Zigo’ wa Ambwene Yessaya ‘AY’
aliomshirikisha Diamond Platinumz wa ‘Zigo’. Tangaza biashara yako hapa. Pia
like page yetu ya facebook Jambo Tz. tu-follow instagram @jambotz.
No comments:
Post a Comment