NI kauli iliyotolewa na Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’
Mbunge wa Jimbo la Mbeya
Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ amesema tukio la kupigwa ngumi na askari
ndani ya Ukumbi wa Bunge lilisababishwa na amri ya Naibu Spika, Job
Ndugai na wala siyo askari.
Aidha Sugu alisema ilikuwa vigumu kuvumilia konde
alilopigwa na askari wakati akitolewa nje kwenye vurugu zilizotokea
bungeni hivi karibuni, ndiyo maana aliamua kulipiza kisasi kwa kutaka
kumpiga ngumi na si kichwa kama anavyodai askari.
‘Sugu’ alitoa kauli hiyo wakati akiwahutubia
wakazi wa Chunya Mjini kwenye mkutano wa hadhara ulioongozwa na Katibu
Mkuu wa Chadema Taifa, Dk Willibrod Slaa ambapo viongozi hao wapo
ziarani mkoani Mbeya wakifanya mikutano na wananchi kwa lengo la
kuwaeleza ukweli wa kilichomtokea Sugu na wabunge wengine bungeni hivi
karibuni.
‘ Sugu’ alidai kuwa Ndugai ni adui wa wapinzani
bungeni na kwamba kwa vyovyote vile ilikuwa vigumu kuvumilia kwa mtu
yeyote baada ya askari kuanza kupiga wabunge kutokana na amri ya
Ndugai.
Naye Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Slaa akizungumzia
suala hilo alisema kitendo alichofanyiwa Sugu hakikuwa kibaya kwake peke
yake, bali hata wananchi waliomchagua.
Hata hivyo, Dk Slaa alisema kwa upande mwingine
ili heshima ya Bunge lolote lile duniani iwepo, ni lazima wabunge
watandikane makonde ndani ya Bunge na si vinginevyo hivyo hashangai kwa
kilichotokea kwa Sugu bungeni. Tembelea http://jambotz8.blogspot.com/ kila siku.
Dk Slaa, alimjia juu Ndugai akisema alikiuka
Kanuni za Bunge kwa kitendo hicho na kubainisha kwamba kanuni za Bunge
zipo wazi kabisa kwamba iwapo itatokea vurugu ndani ya Bunge
anachotakiwa kukifanya ni kuahirisha Bunge kwa wakati huo.
Pia alisema askari ambao ni wapambe wa Bunge
‘Sargent at arms’ ndio wenye mamlaka ya kuingia ukumbini na endapo
itatokea nguvu ya ziada hao ndio wanaotakiwa kisheria na siyo kuwaita
askari wa nje ya Bunge kuingia ndani.
Dk Slaa alisema kitendo kilichofanywa na Sugu
pamoja na wabunge wengine ni cha kijasiri na aliwataka kutokurudi nyuma
na misimamo yao bali waendelee kusonga mbele.
1 comment:
uhuni mtu mzima unasema ili heshma irudi bungen lazm watandikane harafu wakitandikana nini kitokee
Post a Comment