Sunday, April 19, 2015

ALIYENUSURIKA AJALI MBEYA ASIMULIA..!!!

Mmoja wa manusura  wa ajali iliyotokea eneo la Mto Kiwira, Rungwe mkoani Mbeya, Mariam Manfredy akiwa amelazwa kwa matibabu katika  Hospitali ya Rufaa Mbeya. 

Mmoja wa majeruhi wa ajali iliyoua watu 19, Mariam Manfredy (28) aliyevunjika mguu wa kushoto, anasimulia ajali hiyo na kusema chanzo ni mwendo kasi na kuungua kwa breki.

Gari hilo lilikuwa ‘limeshona’ abiria, lilikuwa likitoka jijini Mbeya  kwenda Kiwira wilayani Rungwe kabla ya kuanguka eneo la Mto Kiwira na kuua watu 18 palepale na mmoja alifia Hospitali ya Igogwe huku wengine watatu wakijeruhiwa.

Mariam aliyelazwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya (MRH), alisema alipanda basi hilo katika Kijiji cha Simambwe akienda Kiwira kununua bidhaa za biashara. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

MADEREVA WA MABASI KAMA WA BODABODA...!!!

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, akitoa takwimu za vifo vilivyotokana na ajali za barabarani kati ya Januari Mosi mwaka huu hadi Aprili 12, sawa na siku 102 vifo 969.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, akitoa takwimu za vifo vilivyotokana na ajali za barabarani kati ya January Mosi hadi Aprili 12 mwaka huu, sawa na siku 102 vifo 969.

WAKATI ajali za barabarani zikiendelea kumaliza nguvu kazi ya Taifa na kuumiza vichwa vya Watanzania kuhusu suluhisho la ajali hizo, imefahamika moja ya tatizo sugu ni kukosekana kwa madereva wenye taaluma stahiki, ingawa wana leseni.

Wiki hii peke yake, ajali tatu za mabasi zilizotokea Mbeya, Morogoro na maeneo ya Mwanza, zimesababisha vifo vya watu 40 ndani ya siku sita.

Tayari Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, ametoa takwimu za vifo vilivyotokana na ajali za barabarani kati ya Januari Mosi mwaka huu hadi Aprili 12, sawa na siku 102 vifo 969. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

SOMA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI APRILI 19, 2015 YA DINI, MICHEZO NA HARD NEWS

DSC01499
DSC01500
DSC01501 
Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

UWT ARUSHA WAWAKATAA WALIMU KUSIMAMIA UCHAGUZI MKUU

Wanawake wa UWT wakishangilia.
Wanawake wa UWT wakishangilia.

JUMUIYA ya Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Arusha, imetangaza wazi kuwakataa walimu kusimamia uchaguzi wa madiwani, wabunge na rais, kutokana na tabia ya kufanya hujuma kwa chama hicho wakati wanasaidiwa mambo mengi ya msingi na serikali ya CCM.
Mbali ya walimu, pia UWT imewanyooshea kidole baadhi ya polisi mkoani Arusha kwa kuwa na mapenzi yaliyopitiliza dhidi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), hali inayowafanya kushindwa kutenda haki katika maamuzi mbalimbali.

Msimamo huo umetangazwa kwa nyakati tofauti na Mwenyekiti wa jumuiya hiyo mkoa wa Arusha, Flora Zelote alipokuwa akizungumza katika kata mbalimbali za wilaya ya Arusha katika ziara yake ya kikazi ya kukagua uhai wa jumuiya hiyo na chama kwa ujumla. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

USALAMA WAIMARISHWA AFRIKA KUSINI

Ubaguzi dhidi ya wageni nchini Afrika kusini 
 
Maafisa zaidi wa polisi wametumwa katika maeneo yenye mashambulio dhidi ya raia wa kigeni nchini Afrika Kusini. Yamkini watu sita wameuawa na makundi yenye silaha, ambayo yanawalaumu wahamiaji wa kiafrika kwa kuchukua kazi zao nchini Afrika Kusini.

Rais Jacob Zuma amewatembelea watu hao walioathirika na ghasia hizo, mauwaji pamoja na kuibwa kwa mali zao huku akiahidi kukabiliana vilivyo na wimbi la mashambulio hayo.
Bwana Zuma alifutilia mbali ziara yake nchini Indonesia, ili kukabiliana na vurumai hizo zilizoanza majuma mawili yaliyopita.

Yamkini watu sita wameuawa na makundi yenye silaha, ambayo yanawalaumu wahamiaji wa kiafrika kwa kuchukua kazi zao nchini Afrika Kusini. Nchini Harare Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, alilaani ghasia hizo.

Ghasia hizo zilianza baada ya mfalme mmoja wa Kizulu, Goodwill Zwelethini, kusema kuwa raia wa kigeni sharti waondoke Afrika Kusini. Akiongea katika kambi hiyo iliyoko mjini Durban kiongozi mkuu wa jimbo la Gauteng, David Makhura, anasema kuwa uhasama na ghasia hizo zinazoshuhudiwa, haundamani na uhuru wa miaka mingi ambayo Afrika Kusini ilipigania. Tangaza biashara yako hapa kwa bei nafuu zaidi, pia usisahau ku-Like Ukurasa Wetu Wa Facebook Kwa Kubofya/ Click Neno Jambo Tz.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...