Thursday, September 11, 2014

UKAWA WAPAZA SAUTI...!!!

 
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbroad Slaa akizungumza na wenyeviti wenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), James Mbatia (kulia) na Ibrahim Lipumba baada ya kumaliza kuzungumza na waandishi wahabari kuhusu mchakato wa Katiba na Uchaguzi Mkuu wa 2015.

Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), umemtaka Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba (BMK), Samuel Sitta kusitisha vikao vya Bunge sasa mpaka mwafaka utakapopatikana kwa kuwa kuendelea kwake kunahalalisha ulaji wa fedha za walipakodi.
Akisoma tamko la vyama hivyo mbele ya wanahabari jana, Mwenyekiti mwenza wa Ukawa, James Mbatia, alisema: “Ukawa tunapaza sauti zetu, tukisema hapana! Hapana! Haikubaliki.”
Alisema kwa kuwa Rais Jakaya Kikwete na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), wameafikiana kuahirishwa kwa Bunge hilo kupisha maandalizi ya Bunge la Muungano wa Tanzania, kuendelea kwa BMK hadi Oktoba 4 ni ufujaji wa fedha za umma.
Mbatia alisema TCD walikubaliana kuwa mchakato wa Katiba hauwezi kufikia mwisho sasa kutokana na mambo kadhaa kutokwenda sawa. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

'SARAFU YA SH 500 NI ISHARA MBAYA'




Huo ni uamuzi wa kawaida tu wa kuiongezea uimara wa kukaa muda mrefu kama BoT walivyosema. Kinach opunguza nguvu ya fedha siyo sarafu wala noti...hivyo uchumi tulionao na mfumuko wa bei hatujafikia kiwango cha kusema Shilingi imeshuka thamani,”  Dk Urassa  
Baada ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kutangaza matumizi ya sarafu mpya ya Sh500, baadhi ya wachumi na wadau wa sekta binafsi nchini wamesema hatua hiyo inaashiria kuporomoka kwa thamani ya shilingi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, wachumi hao walisema kuwapo kwa sarafu hiyo inaonyesha uwezo wa Shilingi kununua bidhaa unazidi kupungua.

Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Biashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA), Daniel Machemba alisema Serikali ingejikita zaidi kuzuia kushuka kwa thamani  badala ya kuongeza sarafu.

“Kadri unavyoongeza ukubwa wa fedha, ndivyo inavyozidi kushuka thamani. Hii inamaanisha tunakoelekea tunaweza tukawa kama Zimbabwe kuwa na noti hadi ya Sh100 milioni,” alisema Machemba.

Alisema kuna haja ya Serikali kuzuia matumizi makubwa ya fedha za kigeni nchini hususan Dola za Marekani katika taasisi mbalimbali. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS SEPTEMBA 11, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.

.
.
.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MBOWE AWAONYA WATAKAOCHAGULIWA KWA NJIA YA RUSHWA


Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema chama hakitasita kumvua wadhifa yeyote atakayebainika kuchaguliwa kwa kutoa rushwa.

Mbowe alitoa kauli hiyo jana katika Mkutano Mkuu wa Baraza la Vijana wa Chama hicho, (Bavicha) kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa viongozi watakaoliongoza baraza hilo kwa miaka mitano.

“Hatutawavumilia watakaoshinda kwa rushwa, kinachotakiwa ni wanachama kuchagua viongozi watakaokipeleka mbele chama, chagueni vijana makini na watakaokipeleka chama kushinda chaguzi za vitongoji, serikali za mitaa, udiwani, ubunge na hatimaye uchaguzi mkuu,” alisema Mbowe.

Mbowe, ambaye ni Mbunge wa Hai na kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni aliwahadharisha viongozi watakaopatikana kuhakikisha wanakwenda kuendeleza mapambano. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

YONA AANZA KUJITETEA KISUTU



Waziri wa zamani wa Wizara ya Nishati na Madini, Daniel Yona. Picha na Maktaba 

Waziri wa zamani wa Wizara ya Nishati na Madini, Daniel Yona ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa mchakato wa kumpata mkaguzi wa madini ya dhahabu ulifuata utaratibu kwa kusimamiwa na Gavana wa Benki Kuu Tanzania (BoT).

Aliyaeleza hayo jana alipojitetea dhidi ya mashtaka ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia Serikali hasara ya Sh11.7 bilioni yanayomkabili na wenzake wawili.

Akiongozwa na wakili wake, Eliasa Msuya kutoa ushahidi wa utetezi mbele ya jopo la mahakimu watatu wanaoisikiliza kesi hiyo, John Utamwa, Sam Rumanyika na Saul Kinemela, Yona alidai kuwa wakati wakiendelea na utaratibu wa kumtafuta mkaguzi wa dhahabu walipata ushauri kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Alidai kuwa utaratibu wa kumtafuta mkaguzi huyo nchini ulitokana na malalamiko ya wananchi, Bunge, vyombo vya habari na mashirika yasiyo ya kiserikali mwaka 2002, kuhusu mapato ya madini hayo yaliyokuwa yakichimbwa na kampuni tano za kigeni. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

RAIS JONATHAN AAMURU MABANGO YANG'OLEWE

Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan ameamuru mabango ya hekeheka za uchaguzi yenye nembo ya kauli mbiu ya 'Bring Back Jonathan 2015' yang'olewe mara moja.
Mabango hayo yamelaaniwa vikali kwenye mitandao ya kijamii kwani yanaonekana kuiga kauli mbiu iliyotumiwa katika kampeini ya kuitaka serikali kuwaokoa wasichana waliotekwa nyara na wanamgambo wa Boko Haram mwezi Aprili mwaka huu.
Kundi hilo la wapiganaji wa kiisilamu bado linawashikilia wasichana hao, Wakati ambapo mabango ya Bring Back Jonathan 2015 yaliowekwa kando ya barabara kuu mjini Abuja, yalilaaniwan vikali nchini Nigeria na kimataifa kupitia katika mitandao ya kijamii.
Watu walihisi kuwa ilikuwa ni kama kejeli kwa kampeini ya 'Bring Back Our Girls' ambayo ilienea kote duniani baada ya Boko Haram kuwateka nyara wasichana wa shule ya Chibok.
Wasichana hao 219, bado hawajulikani waliko miezi mitano baada ya kutekwa kwao.
Rais Jonathan, ameyataka mabango hayo kuondolewa kwenye barabara za mji haraka iwezekanavyo.
Katika taarifa yake alisema yeye pamoja na wanigeria wengi wanahisi kuwa kampeini hiyo ilikuwa na nia mbaya na kusisitiza kuwa juhudi bado zinafanywa kuwoakoa wasichana hao waliotekwa na Boko Haram. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Na BBC

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...