Friday, June 05, 2015
IDADI YA WALIOFARIKI GHANA YAFIKIA 175
Takriban
watu 175 wamefariki kufiakia sasa kufuatia moto uliotokea katika kituo
kimoja cha mafuta katika mji mkuu wa Ghana Accra.
Moto huo
uliozuka siku ya jumatano usiku ulianza wakati wakaazi wa mji huo
walipokuwa wakikabiliana na siku mbili za mvua kubwa ambayo imewaacha
raia wengi bila makaazi pamoja na stima.
Mafuriko hayo yaliathiri juhudi za uokozi na huenda yalisababisha moto kulingana na mwandishi wa BBC Sammy Darko mjini Accra. Tayari Ghana imetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kufuatia vifo hivyo.
Mlipuko huo ulitokea hapo jana
wakati mamia ya watu walipokuwa wamejihifadhi katika kituo hicho cha
mafuta kutokana na mvua kubwa zinazonyesha. Rais wa Ghana, John Mahama amesema janga hilo halitajirudia tena.
RAHEEM STRLING KUELEKEA OLD TRAFFORD
Mshambuliaji
wa Liverpool Raheem Sterling huenda akaelekea katika kilabu ya
Manchester United ,hatahivyo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 ana
wasiwasi kuhusu athari za uhamisho huo hususan kutokana na ushindani
mkali uliopo kati ya klabu hizo mbili.
Sterling amekataa ombi la kitita cha pauni laki moja kutoka kwa Liverpool akisema kuwa anataka kuondoka na kukichezea kilabu ambacho kina uwezo wa kushinda mataji. Nunua gari bei rahisi bofya hapa.
SERENA ATINGA FAINALI FRENCH OPEN 2015
Serena
Williams amefanikiwa kutinga fainali za michuano ya tenis ya French
Open. Licha ya kujisikia kuumwa Serena aliweza kupambana vikali na
kumbwaga mpinzani wake Timea Bacsinszky kwa seti 4-6 6-3 6-0 na kufuzu
kucheza fainali za mwaka huu.
Serena nambari moja duniani kwa wanawake sasa atapambana na Lucie Safarova katika mchezo wa fainali kesho, Jumamosi. Serena amekuwa akiumwa kipindi chote cha michuano hiyo, kiasi kwamba anasema hakutarajia kushinda katika mchezo huo.
Serena anajaribu kushindi taji la tatu la michuano hiyo ya French Open na taji la ishirini la michuano mikubwa. Mapema
katika uwanja wa Philippe Chatrier, Safarova wa 13 kwa ubora alimtupa
nje MSerbia Ana Ivanovic na kuwa mwanamke wa kwanza wa Czech kufika
fainali za michuano hiyo katika uwanja wa Roland Garros katika kipindi
cha miaka 34.
Kwa upande wa Wanaume, fainali zitafanyika Jumapili hii. Nunua gari bei rahisi bofya hapa.
Subscribe to:
Posts (Atom)