Sunday, July 28, 2013

MAGAZETI YA LEO JUMAPILI JULAI 28, 2013

DSC 0002 7d9bd
DSC 0003 f899b

LULU MICHAEL..... "SASA NIMEOKOKA.....UJINGA SITAKI TENA"


MUIGIZAJI machachari wa filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amesema baada ya kupata misukosuko ya kimaisha, sasa maisha yake ameyaelekeza katika sala kumuomba Mungu amsamehe makosa yake. 
Lulu alisema hayo juzi, katika kipindi cha Friday Night Live (FNL), kinachorushwa na kituo cha Televisheni cha EATV cha Jijini Dar es Salaam.

“Sasa hivi nasali sana, namuamini Mungu katika maisha yangu na mbali ya kwenda kanisani, pia nasali mwenyewe katika sala zangu.

“Ningependa maisha ya sasa ninayoishi ningeishi siku za nyuma, lakini yote ya Mungu labda maisha yale nisingeyaishi siku za nyuma, ningekuja kuyaishi baadaye,” alisema Lulu.

Katika hatua nyingine, alisema anavutiwa na kazi ya msanii wa bongo fleva, Bernard Paul ’Ben Pol’ ambaye tungo za nyimbo zake zinamkosha kuzisikiliza.

SKENDO KUHUSU KUHUSU NIVA NA WEMA SEPETU KUWA WAPENZI HIKI NDICHO ALICHOKISEMA NIVA.

Siku za hivi karibuni mwigizaji anayefanya vizuri kwasasa katika filamu nchini Niva Zubery amekuwa akiweka status zikimhusu mwigizaji mwenzake Wema Sepetu na baadhi ya mashabiki wa mastaa hao na wasomaji wa Swahiliworldplanet kutaka kuupata ukweli kama mastaa hao ni wapenzi kwa siri au lah. "nyie swp  hembu muulizeni Niva kama mtu wake kwasasa ni Wema coz status zake ni za kuchombeza kwa bibieee then kama wako close sana siku hizi, maskini kaka wa watu kaoza kwa wema tayariii !" alisema shabiki mmoja wa kike aliyekataa kutajwa jina lake.  Status za Niva zinaonekana kama kuchombeza kitu flani kwa Wema kwa mujibu wa wasomaji walioitonya SWP. Baadhi ya status hizo za Niva katika facebook yake ni hizi hapa "Baaabaa eti wewe upo na wemaa? (Apana mwanangu) huku akiwa ameweka picha yake mwenyewe na ya mtoto anayedaiwa kuwa wake", nyingine iko hivi "Niva hanipokerei cm jamaani mwambieni basi kama nampigiaa mwambieeni nawaomba tafazalii" huku akiwa amepost picha ya Wema Sepetu akiwa ameweka simu sikioni".
Status nyingine akiwa ameweka picha hiyo hapo chini wakiwa pamoja na Wema ilisomeka hivi "Etiiiiiii kama tunamuaa kuwa nanihiii na nanihiii itakuwa poa? basi nipe maoni yako ili nijue simmeshajua nilicho maanisha so nataka jibu ili nijue". Baadhi ya wachangiaji walimwambia Niva kuwa wakiwa wapenzi yeye na Wema watapendeza huku wengine wakimwambia kuwa Wema sio hadhi  yake, wengine walimwambia ajaribu bahati yake kama tayari ameshamzimikia mrembo huyo. Ili kuupata ukweli kutoka kwa Niva mwenyewe kama baadhi ya wasomaji walivyotutumia ujumbe mwanzoni ilibidi kumtafuta Niva jana na kumueleza kila kitu na yeye alikataa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Wema na alipoulizwa kama kweli sio wapenzi status zake zikionekana kwa mtu wa Wema si zinaweza kuzua tafrani? Niva alijibu kwa ufupi kwa kusema "hakuna kitu kama hicho kaka"
                                                             Niva na Wema

GADNA AFUNGUA MILANGO KWA WASANII


MTANGAZAJI aliyejizolea umaarufu kupitia kipindi chake cha Maskani kinachorushwa katika kituo cha redio Times, Gadna G. Habashi ameweka mikakati ya kutoa nafasi ya kucheza muziki wa kizazi kipya ndani ya kipindi hicho bila ya kuchagua.

Gadna ambaye anaamini kuwa kipindi cha redio kinapendezeshwa kwa kupiga muziki, hivyo kwa upande wake anaamini kipindi chake kinaboreshwa na muziki hususani wa bongo fleva.


Mtangazaji huyo aliweka wazi juu ya mikakati hiyo alipozungumza na mwandishi wa habari hizi, ambapo alisema njia hiyo ni moja ya mikakati yake ya kutoa fursa kwa wanamuziki wa hapa nchini, ambayo inaonekana wengine wanakosa kwenye redio nyingine.


"Unajua mimi nisipopiga muziki kipindi hakipendezi, hivyo nikipiga muziki huo kwanza ni njia ya kuutangaza muziki pamoja na msanii mwenyewe bila ya kubagua muziki huu ni wa nani?" alisema Gadna.


Alisema kwenye kipindi chake hachagui ni mwanamuziki gani apige nyimbo zake, bali anachokifanya ni kuangalia jamii inahitaji burudani ya aina gani.


Gadna ni mtangazaji anayeamini kuwa neno la kutoa fursa linaendana na vitendo, hivyo moja ya kitendo anachokiamini kinachowasaidia wasanii nyumbani ni kupiga nyimbo zao kwenye redio, ili kumuwezesha msanii afahamike na aweze kupata shoo.

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...