Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa (katikati)
akiangalia dawa za kulevya aina ya heroine zilizokamatwa nchini,
zikifunguliwa na afisa wa jeshi la polisi Neema Mwakagendi kabla ya
kuteketezwa jana, katika tanuri la Kiwanda cha Saruji wazo jijini Dar es
Salaam.Dawa aina mbalimbali zilizokamatwa ziliteketezwa. Picha na
Juliana Malondo
********
Watanzania wawili wanahojiwa na Polisi wa Afrika Kusini baada ya kukamatwa jana na kilo 55 za dawa za kulevya.
Watu hao wawili wanatazamiwa kufikishwa mahakamani
kesho kujibu tuhuma za kukamatwa na dawa hizo zenye thamani ya Rand75
milioni (Sh11.7 bilioni).
Maofisa wa Kikosi Maalumu cha Kupambana na Makosa
ya Jinai na Rushwa cha Afrika Kusini (The Hawks), kiliwakamata watu hao
katika Kitongoji cha Kempton Park, Ekurhuleni, Jimbo la Gauteng.