Kijana Daniel Kossam (21) anayetuhumiwa kumuua bosi wake Bi. Pelesi Chaula (32) akiwa chini ya polisi kwenda kuonyesha pesa na simu alivyotumbukiza chooni.
Marehemu Bi. Pelesi Chaula (32) enzi za uhai wake
Na Uswege Luhanga
Kijana Daniel Kossam (21) anatuhumiwa wa kumuua bosi wake Bi. Pelesi Chaula (32) ambaye alikuwa akiishinaye nyumba moja huko mtaa wa Ilembo kata ya Iyela mkoani Mbeya. Daniel alikuwa akiuza duka la vifaa vya pikipiki la bi. Pelesi lijulikanalo kwa jina la 'Twiyanze' lililopo kijiji cha Mbalizi nje kidogo ya jiji la Mbeya.
Chanzo cha ugomvi inadaiwa kuwa ni
kuchelewa kurudi nyumbani kijana huyo ndipo Pelesi alipochukua jukumu la
kumuuliza jambo lililozua ugomvi katiyao na kusababisha kifo cha
bi. Pelesi Chaula. Kifo cha marehemu Pelesi kimetokana na kupigwa na kitu chenye ncha kali mwilini mwake. Wakati mauaji hayo yanafanyika mume wa bi Pelesi Chaula alikuwa safarini wilayani Makete mkoani Iringa.
Baada ya mauaji hayo Kijana Daniel
alichukua simu mbili za marehemu na simu yake pamoja na fedha kiasi cha
114, 000/= na kuzitumbukiza chooni kisha alienda kwa jirani kuwajulisha
kuwa walikuwa wamevamiwa na majambazi na kwamba wamemuua bosi wake huyo.
Majirani walipofika eneo la tukio
walishangaa kuona kuwa hakuana sehemu ya nyumba iliyokuwa imevunjwa,
walipo muuliza Daniel alijibu kuwa alisahau kufunga milango, baaada ya
majibu hayo waliingiwa na mashaka na kuamua kutoa taarifa polisi.
Akizungumza na mwandishi wa habari
hizi Mjumbe wa serikali ya mtaa Bi. Neema Mwasampeta alisema, 'Dan
alichelewa kurudi na alifokewa sana,nadhani hicho ndiyo chanzo cha
ugonvi wao'. Aliongeza kuwa alimjua kijana huyo kwa muda wa mwaka mmoja.
No comments:
Post a Comment