ILIKUWA Novemba 28, mwaka 2011, Arsenal ilipoondoka imetota vibaya Uwanja wa Old Trafford ikitandikwa mabao 8-2, siku ambayo Wayne Rooney alifunga Hat-trick na Ashley Young akafunga mawili. Danny Welbeck pia alifunga.
Kwa kiasi kikubwa Arsenal imekuwa ikinyanyaswa na Mashetani hao Wekundu, wakiwa wameweza kushinda mechi moja tu ndani ya misimu 10 na wao wakifungwa mechi 11.
Man United 2-1 Arsenal, Ligi Kuu Novemba 3, 2012
Van Persie alihitaji dakika tu kuwakumbusha mashabiki wa Arsenal kipi watakosa kwa kuuzwa kwake kwa Pauni Milioni 24 kwenda Old Trafford, akifunga bao la kwanza kwa guu la kulia. Patrice Evra akaifungia la pili United baada ya mapumziko na Santi Cazorla akaipatia bao la kufutia machozi Arsenal. Kipigo hicho kiliwaacha Arsenal na pointi 15 baada ya mechi 10, mwanzo mbaya zaidi katika historia yao kwenye Ligi Kuu ya England chini ya Wenger.
Man United 8-2 Arsenal, Ligi Kuu Novemba 28, 2011