ILIKUWA Novemba 28, mwaka 2011, Arsenal ilipoondoka imetota vibaya Uwanja wa Old Trafford ikitandikwa mabao 8-2, siku ambayo Wayne Rooney alifunga Hat-trick na Ashley Young akafunga mawili. Danny Welbeck pia alifunga.
Kwa kiasi kikubwa Arsenal imekuwa ikinyanyaswa na Mashetani hao Wekundu, wakiwa wameweza kushinda mechi moja tu ndani ya misimu 10 na wao wakifungwa mechi 11.
Man United 2-1 Arsenal, Ligi Kuu Novemba 3, 2012
Van Persie alihitaji dakika tu kuwakumbusha mashabiki wa Arsenal kipi watakosa kwa kuuzwa kwake kwa Pauni Milioni 24 kwenda Old Trafford, akifunga bao la kwanza kwa guu la kulia. Patrice Evra akaifungia la pili United baada ya mapumziko na Santi Cazorla akaipatia bao la kufutia machozi Arsenal. Kipigo hicho kiliwaacha Arsenal na pointi 15 baada ya mechi 10, mwanzo mbaya zaidi katika historia yao kwenye Ligi Kuu ya England chini ya Wenger.
Man United 8-2 Arsenal, Ligi Kuu Novemba 28, 2011
Kipigo cha 'mbwa mwizi' kilichotoka na
Rooney kufunga hat-trick United ikijibu kipigo cha Manchester City cha
5-1 msimu huo. Ikiwa imeathiriwa zaidi na majeruhi na wachezaji kuwa nje
wakitumikia adhabu, Arsenal ilikuwa dhoofu haswa. Hakika ilikuwa moja
ya siku mbaya sana kwa Wenger kazini. "Tulivunjika nguvu kipindi cha
pili, ni maumivu makubwa,"alisema kocha huyo wa Arsenal.
Bao tamu la kichwa la Ji Sung-Park
lilitosha kuizamisha Arsenal mbele ya United, siku ambayo mchezaji mpya
wa Gunners Marouane Chamakh alipoteza nafasi nzuri.
Man United 2-1 Arsenal, Ligi Kuu, Agosti 29, 2009
Man United 2-0 Arsenal, KOmbe la FA, Machi 12, 2011
Pamoja na Arsenal kutawala sana mchezo, mwisho wa siku walichapwa. Wauwaji siku hiyo walikwa Fabio da Silva na Rooney.
Man United 1-0 Arsenal, Ligi Kuu, Desemba 13, 2010
Man United 2-1 Arsenal, Ligi Kuu, Agosti 29, 2009
Siku hiyo Arsenal walianza vizuri,
Andrey Arshavin akitangulia kuwafungia bao la kuongoza. Bao
lilisawazishwa baada ya kipa Manuel Almunia kumchezea rafu Rooney kwenye
eneo la hatari aliyekwen kufunga kwa penalti. Abou Diaby akajifunga
mwenyewe dakika tano baadaye kuipa United bao la ushindi. Wenger
akapandishwa jukwaani baada ya kutupa chupa dakika ya 95, kufuatia bao
zuri la kusawazisha lililofungwa na Van Persie kukataliwa akiambiwa
aliotea.
Man United 0-0 Arsenal, Ligi Kuu Mei 16, 2009
Arsenal ilikwenda Old Trafford kwa
lengo la kuwabania United wasitwae taji mapema, baada ya kuwa tayari
wamebeba taji la Ligi ya Mabingwa mwezi uliotangulia. Lakini pamoja na
yote, United walipata ponti waliyoihitaji kubeba taji la 11 la Ligi Kuu
wakiwa wamebakiza mechi moja – pia wakafikia rekodi ya Liverpool kutwaa
mtajai 18 jumla ya ligi hiyo tangu inaitwa Daraja la Kwanza.
Man United 1-0 Arsenal, Ligi ya Mabingwa, Aprili 29, 2009
Arsenal walikuwa wenye bahati sana
kufungwa bao moja siku ambayo United walishindwa kutumia vizuri nafasi
walizotengeneza kwa matunda ya kucheza vizuri. Timu ya Ferguson
ilipeleka sukrani zake kwa John O'Shea kuwasogeza jirani na fainali ya
Ligi ya Mabingwa. Arsenal ilitumai kuzinduka katika mchezo wa marudiano
nyumbani, lakini siku hiyo hawakufanya kosa baada ya kukifumua kikosi
cha Wenger mabao 3-1 na kuifuata Barcelona katika fainali.
Man United 2-1 Arsenal, Ligi Kuu, Aprili 13, 2008
Arsenal ilipata nafasi lakini
ikashindwa kuitumia kuimaliza United, baada ya Adebayor kuwafungia bao
la kuongoza dakika mbili baada ya mapumziko ingawa mkono ulihusika
katika bao hilo hilo. United ilisawazisha kupitia kwa Ronaldo kwa
penalti baada ya William Gallas kuunawa mpira kwenye eneo la hatari,
kabla ya Owen Hargreaves kuifungia United bao la ushindi kwa shuti la
mpira wa adhabu umbali wa mita 25 na kuifanya ipae kileleni kwa pointi
sita zaidi.
.
Man United 4-0 Arsenal, Kombe la FA, Februari 16, 2008
Ferguson aliamua kuwapumzisha Ronaldo
na Ryan Giggs, lakini Rooney alitosha kuwamaliza akifunga bao la kwanza
wakati Darren Fletcher alifunga mawili na Nani moja. Rooney
alijitengenezea nafasi katika kikosi cha kocha wa England wakati huo
Fabio Capello, huku United ikitinga Robo Fainali, ambako kwa bahati
mbaya walitolewa na Portsmouth walioibuka mabingwa.
Man United 0-1 Arsenal, Ligi Kuu Septemba 17, 2006
Baada ya kucheza mechi tatu bila
kushinda tangu mwanzo mwa msimu, Arsenal ilizinduka zikiwa zimebaki
dakika tano mchezo kumalizia, Fabregas alipompokonya mpira Cristiano
Ronaldo kabla ya kumpasia Emmanuel Adebayor ambaye alimtungua Tomasz
Kuszczak. Pamoja na hayo mwisho wa msimu, United iliibeba taji kutoka
kwa Chelsea huku Arsenal ikiachwa kwa ponti 21 nafasi ya nne.
Man United 2-0 Arsenal, Ligi Kuu, Aprili 9, 2006
Mabao ya Rooney na Ji-Sung Park
yalitosha kuimaliza Arsenal huku United ikiweka rekodi ya kushinda mechi
a tisa mfululizo katika ligi.
Man 1-0 Arsenal, Kombe la Ligi, Desemba 1, 2004
Manchester United kwa mara nyingine
waliitambia Arsenal iliyokuwa imesheheni makinda waliosajiliwa na Wenger
kama Robin van Persie wakati Ferguson alikuwa ana wakali kama
Eric-Djemba Djemba na Kleberson. Mchezaji mwingine ambaye hakufika
mbali, David Bellion, ndiye aliyefunga bao hilo pekee sekunde ya 19.
Man United 2-0 Arsenal. Ligi Kuu Oktoba 24, 2004
Van Nistelrooy alitangulia kufunga
dakika ya 72 kwa penalti, na Rooney akafunga la pili dakika ya 90
kumaliza rekodi ya Arsenal kutofungwa ndania ya mechi 49.
Man United 0-0 Arsenal, Ligi Kuu Septemba 21, 2003
Mechi kali ndani ya Old Trafford.
Baada ya dakika 80 mechi ilichafuka baada ya Ruud van Nistelrooy
kuonyeshana ubabe na Patrick Vieira. Kisha katika dakika za lala salama
Van Nistelrooy alikosa penalti baada ya Martin Keown kumchezea rafu
Diego Forlan.
Hiloo: Martin Keown akimzomea Ruud van Nistelrooy baada ya Mholanzi huyo kukosa penalti
Chanzo:bongostaz
No comments:
Post a Comment