SIMBA imepanga kuongeza kiungo
mkabaji, beki wa kati na mshambuliaji kwenye dirisha dogo la usajili
ingawa pia imedai itaangalia kwa jicho la tatu nafasi ya kipa
inayoonekana kusuasua.
Kocha Msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelu 'Julio' alisema nafasi hizo ndizo zimeonekana zina mianya.
Julio, ambaye kikosi chake kina wachezaji 26 alisema wanahitaji kujipanga upya na watawasilisha mapendekezo yao kwa uongozi.
"Tumesuasua katika baadhi ya mechi na
nafasi ambazo tunaweza kuongeza dirisha dogo ni mshambuliaji mmoja, beki
wa kati na kiungo mkabaji ingawa pia tutaangalia nafasi ya kipa, nayo
tunaweza kuongeza nguvu kwani pia inasuasua," alisema Julio, ambaye
habari za ndani zinadai huenda naye akatolewa kwenye benchi la ufundi la
timu hiyo.
Simba ilifanya vizuri katika mechi
kadhaa za mzunguko wa kwanza ingawa ilikuja kupepesuka na kutoka
kileleni ikagota nafasi ya nne.
Hata hivyo Julio alitetea uamuzi wao
wa kuwapeleka wachezaji walioshuka viwango kwenda timu ya vijana baada
ya baadhi ya mashabiki na wanachama kuponda mfumo huo.
"Hatuwezi kuacha jambo hilo, litaendelea hivyo hivyo hata kama hawataki, kwani ndiyo funzo la wachezaji wasiotaka kujituma.
Mchezaji ukishindwa kuonyesha kiwango
unaenda timu B ili upandishe kiwango chako na ukipelekwa kule wale
waliobaki timu kubwa lazima nao watajituma zaidi,"alisema Julio, ambaye
ni mchezaji wa zamani wa Simba.
No comments:
Post a Comment