Kamati
ya utendaji ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya
Nachingwea mkoani Lindi, imemsimamisha Katibu wake, Jordan Membe, kwa
madai ya kwenda kinyume na katiba ya Chama.
Habari kutoka wilayani humo zilizothibitishwa na uongozi wa chama hicho, ngazi ya wilaya na ile ya mkoa, zinaeleza Membe amesimamishwa kutokana na
kukiuka maadili ya uongozi, ikiwa ni pamoja na kujihusisha na masuala ya kuleta na
kusababisha vurugu ndani ya chama.
Baadhi ya wajumbe waliohudhuria kikao hicho, kilichofanyika makao makuu ya ofisi ya chama hicho, wilayani Nachingwea, ambao hawakupenda majina yao kuandikwa kwenye vyombo vya habari kwa madai sio wasemaji wa Chama, wameeleza kuwa Membe anadaiwa kusambaza waraka unaopinga kuondolewa kwa aliyekuwa Naibu Katibu mkuu, Zitto Zuberi Kabwe na wenzake.

Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-like page ya facebook ya Jambo Tz