Ofisa
Mtendaji Mkuu wa MeTL GROUP, Mohammed Dewji (Mb) (wa pili kushoto) na
Mkurugenzi Mtendaji wa Rand Merchant Bank (RMB), Bw. Bruce Macfarlane
(wa pili kulia) wakitiliana saini ya mkopo huo wa bilioni 300 za
kitanzania. Kushoto ni Makamu wa Rais wa MeTL GROUP, Vipul Kakad na
kulia ni Gregory Havermahl wa RMB wakishuhudia tukio hilo la utiliaji
saini wa mkopo baina ya RMB na MeTL Group.
Kampuni
ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL) imetiliana saini
mkataba na benki ya Rand Merchant (RMB) ya Afrika Kusini utakaoiwezesha
kupata mkopo wa zaidi ya sh bilioni 300. Mkataba huo umetiwa saini
nchini Afrika Kusini na Ofisa Mtendaji Mkuu MeTL GROUP, Mohammed Dewji.
Akizungumza
kabla ya kutiwa saini kwa mkataba huo,Dewji alisema kwamba mkataba huo
wa kihistoria unatokana na RMB kuiamini kampuni yake ya MeTL tangu
walipoanza mahusiano ya kibiashara mwaka 2007.
“MeTL
na RMB tulianza mahusiano yetu mwaka 2007, wakati RMB ilipotukopesha
dola za Marekani milioni 7.5million. Wakati huo MeTLilikuwa na bidhaa
mbili tu,ngano na sukari! Toka wakati huo, MeTL imekuwa ikikua na
kuongeza bidhaa zaidi.” Alisema Dewji na kuongeza kuwa mwaka jana 2013,
uwezo wa MeTL wa kukopa sasa umefikia dola milioni 100. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz