Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema wateja wake wote wanaotumia mita za malipo ya kabla yaani (LUKU) kuwa, kuanzia April 2, mwaka huu shirika hilo itahamia rasmi katika mfumo wa malipo wa Serikali ujulikanao Government e-Payment Gateway (GePG).
Mfumo utaanza kutumika kutokana na matakwa ya sheria kwa taasisi za Serikali. Taarifa ya Ofisi ya Uhusiano ya TANESCO makao makuu imeeleza kuwa shirika hilo ni miongoni mwa Taasisi za Serikali, hivyo itaanza kutumia mfumo huu kwa kufanya mauzo ya LUKU kupitia ofisi zake kampuni za simu pamoja na benki zote zinazofanya mauzo ya LUKU kupitia huduma za kibenki.
"Serikali kwa kushirikiana na wataalamu wa TANESCO itahakikisha kuwa mfumo huu unafanya kazi bila kuathiri manunuzi ya LUKU. Ifahamike TANESCO ni miongoni mwa Taasisi za Serikali zitakazotumia mfumo huu mpya na hadi hivi sasa taasisi nyingine za Serikali zimeshaanza kutumia kwa mafanikio.