Thursday, August 07, 2014

MBUNGE CHADEMA ATINGA BUNGENI...!!!

Mbunge wa Viti Maalumu, Chadema  Leticia Nyerere akiwa kwenye viwanja vya bunge jana mjini Dodoma. 

Mjumbe mwingine wa Bunge la Katiba kutoka Kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) jana alionekana kwenye Viwanja vya Bunge na alisaini za mahudhurio.
Mjumbe aliyeonekana jana, Leticia Nyerere wa viti maalumu, Chadema, anafanya idadi ya wajumbe waliotinga kwenye viwanja hivyo hadi sasa kufikia watatu baada ya Chiku Abwao (viti maalumu Chadema) kuonekana juzi na Clara Mwatuka (viti maalumu CUF) kuonekana Jumapili.
Nyerere hakuwa akihudhuria vikao baada ya Ukawa kutangaza kususia Bunge mwezi Aprili na jana hakupatika kuzungumzia suala hilo.
Kuonekana kwa mjumbe hao kunaweza kutafsiriwa kuwa ni kubomoka kwa ngome za Vyama vya Chadema, NCCR na CUF vinavyounda umoja huo kwani tangu awali walikubaliana kutoshiriki shughuli za Bunge hadi pale watakapofikia makubaliano ya hoja zao. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

POLEPOLE: 'ANAYEZUIA MIJAALA YA KATIBA AMEPOTEZA SIFA YA KUWA RAIS'

Aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Hamphrey Polepole akizungumza kwenye mjadala wa wazi kuhusu Katiba mpya, uliofanyika jijini Dar es Salaam jana.

Aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Humphrey Polepole amesema makongamano na mijadala inayohusu Katiba mpya yataendelea kwa sababu ni ya lazima pia ni haki ya kikatiba.
Akizungumza kwenye Kongamano la Katiba lilioandaliwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) jana, Polepole alisema mtu anayezuia wananchi kuendelea kuzungumzia Katiba amepoteza sifa za kuwa kiongozi wa nchi.
Huku akishangiliwa na washiriki wa kongamano hilo, Polepole alisema Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi ya kidemokrasia, inayoheshimu haki za binadamu na utawala wa kiraia. Hivyo inashangaza kusikia kuna kiongozi anajaribu kuwafunga mdomo wananchi. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAPENZI YA KWELI: WAAGA DUNIA PAMOJA BAADA YA MIAKA 62...!!!

Don na Maxine Simpson wakiwa hospitalini
Amini Usiamini mapenzi ya kweli bado yapo humu duniani!
Kisa kimoja ambacho kimedhibitishia wengi baada ya wapenzi wawili waliooana na kuishi pamoja kwa takriban miaka 62 walipoaga dunia pamoja.
Don na Maxine Simpson walikuwa wakazi wa mji wa Bakersfield, ulioko jimbo la California, Marekani waliaga dunia saa nne baada ya kushikana mikono hospitalini na kuahidiana penzi lao halitafifia kamwe hata mauti iwapate.
Walikuwa wamelazwa hospitalini kufuatia hali duni ya afya inayotokana na umri wao mkubwa.
Don na Maxine Simpson wakiwa bukheri wa afya
Lakini punde alipoaga Maxine na mwili wake ukaondolewa chumbani walikokuwa wamelazwa pamoja na mumewe Don, zilipata saa nne tu uchungu ulipomzidi Don na akakata roho iliwaendelee kupendana na mkewe ahera.
Mjukuu wao Melissa Sloan aliiambia runinga ya KERO-TV Kuwa Don alimhusudu sana nyanya yake yaani Maxine tangu alipomtupia jicho mnamo mwaka wa 1952 walipokutana katika mashindano ya Bowling.
Wapenzi hao wawili waliooana mwak huohuo na hawajawahi kuachana tangu hata katika mauti.
''Babu yangu alikuwa anatamani kuishi na nyanya yangu na hata baada ya wawili hao kuanza kuugua kutokana na umri wao mkubwa waliwaomba wasimamizi wa hospitali walimolazwa wasiwatenge.''
Don alikuwa na miaka 90 huku mke wake akiwa na miaka 87.
Don na Maxine Simpson walipokutana
''Babu yangu alihudumu kama mwanajeshi katika jeshi la Marekani naye bibi alikuwa ni muuguzi haswa walipokuwa huko Ujerumani ambapo waliwahi kuishi kwa muda mrefu.''alisema mjukuu wao Melissa.
Wamemuacha nyuma mtoto mmoja wa kiume na wajukuu watano.
Je unaamini kuna penzi la kweli ?
Tuwachie jibu lako katika mtandao wetu wa facebook BBCSwahili.com na pia kwenye tweeter @bbcswahili. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Na BBC

BOKO HARAM WASHAMBULIA CAMEROON

Wapiganaji wa Boko haram
Watu wanaodaiwa kuwa ni kundi la Boko Haramu wameshambulia raia na wanajeshi kaskazini mwa Cameroon ambapo watu kumi wanasadikiwa kufariki dunia.
Shambulio hilo linakuja baada ya shambulio jingine la hivi karibu ambapo wapiganaji wa kundi hilo walivuka mpaka kutoka Nigeria na kufanya mashambulizi kadhaa kwa wiki za hivi karibuni nchini Cameroon.
Tayari majeshi kutoka katika ukanda huo yameahidi kupambana na wapiganaji hao wa Boko Haramu walioua watu 4000 wasio na hatia kwa mwaka huu pekee.

Ni shambulizi la mchana la kusikitisha. Waendesha piki piki wanadaiwa kuwa ni wapiganaji wa Boko Haram waliolenga kukishambulia kijiji caha Zigague kaskazini mwa Cameron.
Walimshambulia kiongozi wa jadi wa baadae kurushiana risasi na kundi la wanajeshi wa Jeshi la Cameroon. Mwanajeshi mmoja aliuawa pamona na raia nane.
Kundi hilo pia lilishambulia kituo cha polis.
Katika siku za hivi karibu wapiganaji wa Boko Haramu wamekuwa wakifanya mashambulizi katika nchi ya Cameroon. Kumekuwa na matukio kadhaa ya utekaji nyara jambo lilosukuma jeshi kuanza mapambano ya angani.
Mashambulizi mengi yanayofanywa Boko Haramu yamekuwa yakielekezwa nchini Nigeria ambapo mashirika ya kutetea haki za binadamu yanasema zaidi ya watu 4000 wameuawa kwa mwaka huu pekee.
Karika siku za hivi karibuni, Camerooni, Nigeria, Chad na Niger zilikubalina kuunda jeshi la pamoja la kanda hiyo ili kupambana na wapiganaji hao wa Boko Haramu. Hata hivyo Cameoroon wakati inatafuta namna ya kupambana Boko haram kunaongeza hali isiyo tabirika ya kuongezeka kwa mashambulizi. Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MASOGANGE AHOJIWA ZAIDI YA MASAA 10 'AIRPORT'

http://jambotz8.blogspot.com/
Kikosi Kazi cha Polisi cha Kuzuia Dawa za Kulevya nchini kimemhoji kwa zaidi ya saa 10, msanii Agnes Gerald ‘Masogange’ kuhusiana na tuhuma za kukamatwa na dawa aina ya crystal methamphetamine huko Afrika Kusini, Julai mwaka jana.
Kamanda wa Polisi Kitengo cha Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Gedfrey Nzowa alisema jana kuwa Masogange alianza kuhojiwa juzi usiku baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam akitokea Afrika Kusini.
Nzowa alisema baada ya kuhojiwa, Masogange aliruhusiwa na kwamba yupo huru, ameachiwa bila masharti yoyote.
Kamanda wa Polisi wa Uwanja wa Ndege, Hamisi Selemani naye alithibitisha kuhojiwa kwa msanii huyo akisema: “Hapa kuna kikosi kazi, kila mmoja alimhoji kwa wakati wake lakini kwa upande wa polisi tulimpekua na kumhoji lakini tumemwachia.” Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

MAGAZETI YA LEO ALHAMIS AGOSTI 07, 2014 YA UDAKU, MICHEZO NA HARD NEWS


.

.
.
.
Kuwa wa kwanza kupata habari zetu kwa ku-Like page yetu ya facebook kwa ku-click/ bofya neno Jambo Tz

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...