Thursday, April 05, 2018

CHADEMA WATAJA MAJINA 25 YA WAFUASI WAKE WANAOSHIKILIWA NA POLISI BILA KUPELEKWA MAHAKAMANI

Chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa orodha ya majina ya watu 25, wakiwemo viongozi, wanachama na wafuasi wa wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda ya Dar es Salaam na kuwaagiza wanasheria wake kuchukua hatua zaidi za kisheria kwa kuwasilisha maombi ya ‘Habeas Corpus’, Mahakama Kuu, iwapo jeshi hilo halitawaachia au kuwafikisha mahakamani watuhumiwa hao kama taratibu zinavyotaka.

Chama hicho kimesema kimefikia uamuzi huo, kutokana na tabia ya Jeshi la Polisi kuendeleza utaratibu unaovunja haki na sheria kwa kuwakamata watu na kuwashikilia mahabusu za Polisi kinyume na matakwa ya taratibu za nchi.

Kati ya watu hao 25 wanaoshikiliwa na Polisi, mmoja ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, John Heche, ambaye pia ni Mbunge wa Tarime Vijiji huku watu wengine 24 wakiwemo viongozi, wanachama na wafuasi wa CHADEMA waliikamatwa juzi wakiwa maeneo ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakifuatilia hatma ya dhamana ya viongozi wakuu wa chama mahakamani hapo.

BASI LA CITY BOYS LAGONGANA NA FUSO, 12 WAFARIKI, 46 WAJERUHIWA!

Basi la Kampuni ya City Boys lenye namba za usajili T983 DCE Scania limepata ajali ya kugongana na lori aina ya Fuso lenye namba za usajili T486 ARB katika eneo la Makomero Tarafa na Wilaya Igunga Mkoa wa Tabora usiku wa kuamkia leo na kusababisha vifo vya watu 12 na wengine 46 kujeruhiwa.

Kaimu Mkuu wa Usalama Barabarani wa Mkoa wa Tabora, Insp Hardson, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa chanzo cha ajali hiyo ni tairi la kulia la Fuso lilitumbukia kwenye mashimo mawili na kusababisha tairi kupasuka na rimu kupinda hivyo likakosa mwelekeo na kuligonga basi la City Boy uso kwa uso.

Insp Hardson amesema miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya igunga huku baadhi ya majeruhi wakipelekwa Hospitali ya Nkinga na wengine Bugando Mwanza kwa ajili ya matibabu.

ALIEKUWA RAIS KUFUNGWA MIAKA 12 JELA

Mahakama ya rufaa nchini Brazil leo imeagiza aliekuwa rais wa nchi hiyo, Luiz Inacio Lula da Silva kuwa ni sharti aanze kutumikia kifungo chake cha miaka kumi na mbili gerezani, baada ya kupatikana na hatia ya kuhusika katika ufisadi.
Majaji sita kati ya kumi na mmoja wa mahakama ya rufaa walipinga rufaa hiyo huku watano kati yao wakimuunga mkono. Kesi hiyo imezua hali ya wasi wasi wa kisiasa nchini humo.

Lula amekutwa na hatia kutokana na uchunguzi wa muda mrefu wa sakata la rushwa linalojulikana kama ”Operation Car Wash" Lula aligundulika kukubali rushwa yenye thamani Euro laki 7.

WAZIRI ATAJA HATUA ZINAZOCHUKULIWA NA SERIKALI KUFIKIA UCHUMI WA VIWANDA

 Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Paramagamba Kabudi akizungumza na wadau wa utafiti wakati akifungua Warsha ya siku mbili kwa watafiti wa Tanzania na kutoka nje iliyoandaliwa na Tasisi ya Utafiti ya REPOA jana jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Balozi  Amina Salim Alli akizungumza wakati anaongoza mjadala juu ya Uchumi wa Viwanda kufikia 2025
 
Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi amesisitiza  Serikali ya Awamu ya Tano inaendelea na hatua  za kuhakikisha kunakuwepo mazingira wezeshaji yatayofanikisha ujenzi wa viwanda nchini. 

Prof.Kabudi amesema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akifungua warsha ya utafiti iliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti ya REPOA ambapo mada kuu ilikuwa kujadili kuelekea jamii inayoendeleza viwanda 2025 kwanini ushindani ni muhimu.

Pia kwenye warsha hiyo wadau wamejadili masuala ya kisera katika safari ya Tanzania kuelekea kwenye uchumi mseto na shindani, ukiongozwa na viwanda, pamoja na kufikia nchi yenye kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 kama inavyotarajiwa kwenye dira ya Taifa ya Maendeleo 2025.

ZITTO KUMPELEKA NONDO UHAMIAJI KUHOJIWA

Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe amesema atamsindikiza kiongozi wa mtandao wa wanafunzi Abdul Nondo katika makao makuu ya uhamiaji Tanzania.
Hii ni baada ya taarifa iliotoka mtandao huo ambayo ilieleza kuwa Nondo alipata barua ya kuitwa na uhamiaji ili 'akahojiwe kuhusu taarifa za uraia wake pamoja na za ndugu zake'.

Taarifa hizo zilisema 'afisa uhamiaji mkoa alitamka kuwa sheria inawaruhusu kumuhoji mtu yeyote wanaotilia mashaka uraia wake. Na kuwa wanamashaka na uraia wa Abdul Nondo,hivyo awathibitishie kuwa yeye ni Raia wa Tanzania'.

SOMA MAGAZETI YA LEO ALHAMIS APRIL 05, 2018 YA UDAKU, MICHEZO NA HARDNEWS




Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...