Chama cha Demokrasi na Maendeleo (CHADEMA) kimetoa orodha ya majina
ya watu 25, wakiwemo viongozi, wanachama na wafuasi wa wanaoshikiliwa na
Jeshi la Polisi Kanda ya Dar es Salaam na kuwaagiza wanasheria wake
kuchukua hatua zaidi za kisheria kwa kuwasilisha maombi ya ‘Habeas
Corpus’, Mahakama Kuu, iwapo jeshi hilo halitawaachia au kuwafikisha
mahakamani watuhumiwa hao kama taratibu zinavyotaka.
Chama hicho kimesema kimefikia uamuzi huo, kutokana na tabia ya Jeshi
la Polisi kuendeleza utaratibu unaovunja haki na sheria kwa kuwakamata
watu na kuwashikilia mahabusu za Polisi kinyume na matakwa ya taratibu
za nchi.
Kati ya watu hao 25 wanaoshikiliwa na Polisi, mmoja ni Mjumbe wa Kamati
Kuu ya CHADEMA, John Heche, ambaye pia ni Mbunge wa Tarime Vijiji huku
watu wengine 24 wakiwemo viongozi, wanachama na wafuasi wa CHADEMA
waliikamatwa juzi wakiwa maeneo ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu
wakifuatilia hatma ya dhamana ya viongozi wakuu wa chama mahakamani
hapo.
Aidha kimedai kuwa miongoni mwa watu hao 24, wamo pia wananchi ambao walikuwa
wakiendelea na shughuli zao za kila siku lakini walikumbwa na
kamatakamata hiyo iliyofanywa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Ilala.
Majina ya watu hao 25 wanaoshikiliwa na polisi ni:-
1. John Heche (Mb Tarime Vijijini)
2. Lilian Kumei
3. Jonathan Lema
4. Beatrice Mdanya
5. Charles Kakumbi
6. Neema Nyimbo
7. Elizabeth Tossy
8. Ernest Mbuya
9. Damas Mwita
10.Daniel Mshana
11. Paul Shija
12. Jerry Kerenge
13. Patrick Peter
14. Christina Darabe
15. Adinani Mushi
16. Mbezi Mombeki
17. Jonathan Kimaro
18. Paulo Makali
19. Meshak Mwacha
20. Godfrey Jackson Kayanda
21. Ramadhani Mkude
22. Happy Baega
23. Novatus Tesha
24. Jonathan Robert
25. Fikirini Vicent
CHADEMA wameeleza kuwa wanakwenda mahakamani, ili Mahakama Kuu
iliamuru jeshi hilo na mamlaka zingine zinazohusika, kujieleza kwanini
zinavunja haki na sheria kwa kuendelea kuwashikilia watu hao bila
kuwaachia au kuwafikisha Mahakamani.
No comments:
Post a Comment