Waziri
wa Katiba na Sheria, Profesa Paramagamba Kabudi akizungumza na wadau wa
utafiti wakati akifungua Warsha ya siku mbili kwa watafiti wa Tanzania
na kutoka nje iliyoandaliwa na Tasisi ya Utafiti ya REPOA jana jijini Dar
es Salaam.
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
Balozi Amina Salim Alli akizungumza wakati anaongoza mjadala juu ya
Uchumi wa Viwanda kufikia 2025
Waziri
wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi amesisitiza Serikali
ya Awamu ya Tano inaendelea na hatua za kuhakikisha kunakuwepo
mazingira wezeshaji yatayofanikisha ujenzi wa viwanda nchini.
Prof.Kabudi
amesema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akifungua warsha ya
utafiti iliyoandaliwa na Taasisi ya Utafiti ya REPOA ambapo mada kuu
ilikuwa kujadili kuelekea jamii inayoendeleza viwanda 2025 kwanini
ushindani ni muhimu.
Pia
kwenye warsha hiyo wadau wamejadili masuala ya kisera katika safari ya
Tanzania kuelekea kwenye uchumi mseto na shindani, ukiongozwa na viwanda, pamoja na kufikia nchi yenye kipato cha kati ifikapo mwaka 2025 kama
inavyotarajiwa kwenye dira ya Taifa ya Maendeleo 2025.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Infotech Investment Group LTD, Ali Mufuruki akiongoza
majadiliano ya hali ya biashara kwa sasa katika Warsha ya siku mbili
iliyoandaliwa na Repoa nchini.
Akizungumza baada ya ufunguzi wa washa hiyo Profesa Kabudi ametaja hatua mbalimbali
ambazo Serikali inachukua katika kufanikisha ujenzi wa viwanda nchini
na kufafanua kinachoendelea ni kuangalia jinsi gani kufanya bidhaa za
Tanzania kuwa na ushindani kwenye soko la Dunia.
"Kuna
mambo mengi ya kufanya katika kufanikisha ujenzi wa viwanda nchini. Nikumbushe tu wakati tunapata uhuru tulikuwa na viwanda viwili, hivyo
jukumu la wakati ule ikawa ni kuanza kujenga viwanda na vilijengwa na
kutoa ajira kwa wananchi.
Baadhi
ya Washiriki waliohudhuria Warsha ya siku mbili iliyoandaliwa na Tasisi
ya Utafiti nchini Repoa wakifuatilia mijadala mbalimbali
"Hata
hivyo ilipofika mwaka 1977 baada ya kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika
Mashariki tukarudi nyuma kidogo na baadae tukaingia kwenye vita dhidi ya
Uganda ambapo tulitumia dola za Marekani milioni 5 kwenye vita. Hivyo
tukawa hatuna fedha za kuendeleza viwanda.
"Pamoja
na magumu ambayo tumeyapitia bado leo hii tunavyo viwanda vingi ingawa
jukumu la Serikali ni kujenga viwanda zaidi ili kuboresha maisha ya
wananchi wake katika kuleta maendeleo,"amesema Profesa Kabudi.
Amefafanua
kwenye warsha hiyo wamejadili kwa kina hatua ambazo zinatakiwa
kuchukuliwa katika kufikia malengo la kujenga viwanda na kuboresha
maisha ya wananchi na kutumia nafasi hiyo kueleza tayari Serikali
imeanza kuchukua hatua kadhaa na baadhi ni elimu bure kuanzia elimu ya
msingi hadi sekondari ambayo inatoa fursa ya kuandaa wasomi kwa
maendeleo ya nchi.
Baadhi ya Washiriki waliohudhuria Warsha ya siku mbili iliyoandaliwa na
Tasisi ya Utafiti nchini Repoa wakifuatilia mijadala mbalimbali
Waziri
wa Katiba na Sheria, Profesa Paramagamba Kabudi watatu kushoto akiwa
katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Tasisi ya utafiti nchini Repoa
pamoja na wadau wa utafiti
Pia
amesema jitiahada nyingine zinaendelea katika ujenzi wa miundombinu ya
barabara reli na bandari na kwamba miundombinu hiyo ni muhimu katika
kujenga msingi imara wa kukuza na kuimarisha uchimi wa Tanzania.
Prof.Kabudi
amezungumzia namna ambavyo Serikali imejikita katika kuboresha sekta ya
afya ili kuwa na wananchi wenye afya imara watakaoshiriki kikamilifu
katika kuleta maendeleo ya Taifa letu. Pia amegusia hatua zinazochukuliwa
katika kuongeza nishati ya upatikanaji wa umeme kwa kuanzisha miradi
mikubwa ya umeme na jana Rais John Magufuli amezindua mradi wa umeme wa
Kinyerezi II.
Mkurugenzi
Mkuuu wa Tasisi ya utafiti nchini Repoa Dk Donald Mmari akizungumza
kabla ya kumkaribisha msemaji mkuu katika warsha hiyo ya kwanini
ushindani juu ya viwanda kufikia 2025
Hata
hivyo amesisitiza umuhimu wa ujenzi wa viwanda na kueleza huko nyuma
wakati kukiwa na viwanda vya kutosha wanawake na wasichana wengi
walipata ajira na kuondoa wale ambao wanaonekana wanazurula mtaani.Hivyo
viwanda vikijengwa vitatoa ajira ikiwamo kwa wanawake.
Kuhusu
malalamiko ya kodi kubwa, Profesa Kabudi amesema tayari Rais Magufuli
ameshatoa maelekezo ya kuhakikisha kodi inakuwa yenye unafuu na juzi
juzi amekutana na wafanyabishara kwa lengo la kujadili namna ya kutatua
changamoto zilizopo kwenye sekta ya biashara na uwekezaji nchini, hivyo
kwenye eneo hilo mambo yanakwenda vizuri.
Kwa
upande wa Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko katika Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar Balozi Amina Salim Ali amesema warsha hiyo imekuja
wakati muhimu kwani yapo mambo ya kiseria ambayo yanajadiliwa na
kuangalia namna ya kuboresha mazingira ya kuinua uchumi wa wananchi na
kwa Zanzibar kuna hatua mbalimbali ambazo wamezichukua katika kuboresha
maisha ya wananchi.
Amesema
kwenye eneo la ujenzi wa viwanda, bajeti ya fedha ya mwaka huu kwa
Zanzibar imejikita pia katika kufufua viwanda vya zamani na ujenzi wa
viwanda vipya kulingana na bajeti ya fedha ambayo wameitenga.
Pia
wameamua kuimarisha kilimo cha bahari na katika hilo kuna baadhi ya
vijana wapo nje ya nchi kwa ajili ya kujifunza mambo ya uvuvi hasa kwa
kuzingati Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imenunua meli ya uvuvi kwa
ajili ya kuwawezesha wavuvi.
Amesema
wameimarisha kilimo cha mbogamboga kwani wanatambua kuna nchi za
Uarabuni ambazo zinanunua mbogamboga kutoka Zanzibar huku akielezea
hatua kadhaa ambazo zinachukuliwa na Serikali katika kuinua uchumi wa
wananchi.
Kuhusu
sera ya viwanda, amesema Zanzibar wameweka mikakati ya kuhakikisha
wanaondoa changamoto zilizopo katika sekta ya viwanda na kuelezea namna
ambavyo wameondoa urasimu kwa wanaotaka kufanya bishara na kuwekeza huku
akizungumzia hatua ambazo wamechukua katika kuimarisha sekta ya utalii
visiwani huo kwa kuhakikisha watalii wakienda wanakaa muda mrefu.
Wakati
huo huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Repoa Dk. Donald Mmari amesema pamoja na
kushuhudia ukuaji mzuri wa uchumi wa Tanzania kwa miaka 15 iliyopita,
tafiti zinaonesha viwango vya tija katika sekta nyingi bado ziko chini
na ushindani wake kulinganisha na nchi nyingine duniani bado
haujaridhisha.
"Hata
hivyo Tanzania ina uwezo wa kujiweka katika nafasi kubwa zaidi katika
uchumi wa dunia kwa kujenga uwezo wa ushindani ukiinuliwa na uwepo wa
faida za kipekee ikiwemo eneo la kijiografia, wingi wa rasilimali za
asili na utulivu wa kisiasa na kijamii.
"Lengo
la warsha hii ni kujadili na kupata maoni yatokanayo ma tafiti na
uzoefu wa nchi nyingine ili yatuongoze katika kushiriki na kuchangia
zaidi kwenye juhudi zinazoendelea za kujenga uchumi wa viwanda
ikizingatiwa kuwa mpango wa tatu wa maendeleo wa miaka
mitato (2021/22-2025/26) utajikita katika kuimarisha uwezo wa Tanzania
kushindana na kuongeza ukuaji wa uchumi kupitia mauzo ya nje ya
nchi," amesema Dk. Mmari.
Na Globu ya jamii.
No comments:
Post a Comment