Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe
amesema atamsindikiza kiongozi wa mtandao wa wanafunzi Abdul Nondo
katika makao makuu ya uhamiaji Tanzania.
Hii ni baada ya taarifa iliotoka mtandao huo ambayo ilieleza kuwa Nondo alipata barua ya kuitwa na uhamiaji ili
'akahojiwe kuhusu taarifa za uraia wake pamoja na za ndugu zake'.
Taarifa
hizo zilisema 'afisa uhamiaji mkoa alitamka kuwa sheria inawaruhusu
kumuhoji mtu yeyote wanaotilia mashaka uraia wake. Na kuwa wanamashaka
na uraia wa Abdul Nondo,hivyo awathibitishie kuwa yeye ni Raia wa
Tanzania'.
Taarifa za kupotea kwa Nondo katika mazingira ya kutatanisha
ziliibuka tarehe 6 Machi baada ya Nondo kutuma ujumbe kwa mmoja wa
marafiki zake usiku wa manane akisema kuwa usalama wake uko hatarini.
Hali
hiyo ilipelekea taharuki miongoni mwa wanafunzi wenzake na jamii kwa
ujumla huku wengi wakidhani kuwa Nondo alikuwa ametekwa.
Nondo anatakiwa kurudi uhamiaji tarehe 20 mwezi Aprili na 'kupeleka
cheti chake cha kuzaliwa, cheti cha kuzaliwa cha baba yake, mama yake,
cha bibi na babu mzaa baba na mzaa mama'.
No comments:
Post a Comment