Thursday, December 05, 2013

MECHI YA NANI MTANI JEMBE KUCHEZWA DESEMBA 21

 Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Mussa Katabaro, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro George Kavishe, Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala na Mkurugezi wa Mashindano wa TFF, Saad Kawemba wakioshela alama ya dole baada ya kutangaza Simba na Yanga kucheza mechi ya Nani Mtani Jembe itakayochezwa Desemba 21 jijini Dar es salaam (Executive Solutions)

 Mechi ya Nani Mtani Jembe kati ya Simba na Yanga zinazodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itachezwa Jumamosi, Desemba 21, 2013 saa kumi kamili jioni kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, Meneja wa Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe amesema “Tayari Simba na Yanga zimesaini makubaliano ya kucheza MECHI YA NANI MTANI JEMBE (NANI MTANI JEMBE MATCH). 
Pambano hili  ni zawadi ya kufungia mwaka kwa mashabiki na kila timu imetia sahihi makubaliano kwamba itachezesha kikosi cha kwanza ili kuwapa mashabiki burudani ya uhakika.”
Kavishe aliongeza kuwa mechi hii ni maalum kwa ajili ya kuhitimisha kampeni ya Nani Mtani Jembe ambayo imeendeshwa kwa zaidi ya miezi miwili ikiwapa fursa mashabiki wa timu hizi kuchangia timu zao kila wanapoburudika na bia ya Kilimanjaro Premium Lager.
Kilimanjaro Premium Lager   ilitenga kiasi cha shilingi milioni 100 zinazoshindaniwa na Simba na Yanga kupitia mashabiki wake na tarehe 21 Desemba ndio utakuwa mwisho wa kampeni ya Nani Mtani Jembe ambapo baada ya mechi  fedha hizo zitagawanywa kwa kila timu kulingana na matokeo ya kura za mashabiki na klabu zitajiamulia namna ya kutumia fedha hizo.
Kampeni hii imeleta msisimko mkubwa sana kati ya mashabiki na hadi sasa matokeo ya kampeni hii yanaonyesha kwamba Yanga wanaongoza wakiwa na kiasi cha shilingi milioni 76 huku Simba wakiwa na kiasi cha shilingi milioni 24
Mashabiki wa Simba na Yanga wanaoshiriki katika kampeni ya Nani Mtani Jembe wanaendelea kunufaika zaidi na zawadi kabambe zilizoandaliwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager ili kuongeza msisimko na ushiriki katika kampeni hiyo ambapo mashabiki watatu wa Simba na mashabiki watatu wa Yanga wanajishindia kiasi cha shilingi 300,000/= kila mmoja katika droo zinazofanyika mara moja kila wiki. Droo kubwa itafanyika tarehe 21 Desemba.  Ambapo katika droo hiyo kubwa shilingi milioni 6 zitatolewa kama zawadi kwa washindi wawili -  mmoja shabiki wa Yanga na mwingine shabiki wa Simba ambapo kila mmoja atajishindia shilingi milioni tatu.

No comments:

Pro

PropellerAds

LinkWithin

Soma na Hizi Pia Plugin for WordPress, Blogger...